NINI HUTOKEA BINADAMU ANAPOKUFA?

0:00

MAKALA

🗣️kwanza kabisa lazima tukubaliane ya kuwa sisi sio hii miili yetu ya kifizikia,Bali miili hii ni kibebeo tu cha Roho zetu Yani sisi wenyewe wa ndani.

👉Sote kwa pomoja tunakubaliana na Hoja hii kwa ushahidi wa kila sekunde ,kila dakika ,kila saa na kila siku tukisema🗣️”HUU NI MWILI WANGU ” tukimaanisha sisi(Mimi) sio huu mwili , ni sawa na kusema “hili ni Shati👔 langu” lakini Mimi sio Hilo shati, basi ndivyo kila muda hukubali kwa Kujua ama kutokujua kwamba tunajitenga na huu MWILI Automatically, kwanini? nikwasababu sisi ni ROHO na Huko nyuma tumekubaliana kuwa Roho kisayansi huitwa Nishati/energy

Sote tunafahamu kuwa “energy can neither be created nor destroyed, but can be transformed into another form

👉Ndiomaana waumini wa dini huita MUNGU(super conscious Energy),Kwanini? Kwa sababu ya kutokuwa na mwanzo wala mwisho na kuwa ndani ya kila kitu na kuweko kila mahali , inachokifanya yenyewe nikujibadili badili Katika maumbo na hali tofauti tofauti, ndio maana Dini husema Roho haikuumbwa na haifi Ila IPO wanaenda mbali zaidi wakisema Mungu ni Roho hana umbo.

Wakati tunaangazia maana ya Roho/enegry ni muhimu kutambua kuwa tunapojikana (kutenga) kuwa sisi sio hii MIILI basi lazima Kufahamu miili yetu ni kitu gani amatuseme Binadamu ni kitu gani hasa?

👉BINADAMU ni kiumbe Chenye mwili wa Nyama unaoonekana Kwa macho ya damu na nyama Katika ulimwengu wa tatu (3Dimension) ambayo ni Dunia(sayari)

👉BINADAMU ni kiumbe chenye utashi wa kiwango Cha juu kuliko viumbe vingine Katika ule mpangilio wa kingdom 4 za Ufahamu(consciousness) Binadamu anatawala mineral, plant na Animal kingdoms kwa kuwa Ufahamu wake upo juu kutokana Binadamu ana UBONGO unaoendesha mwili kupitia Ile milango 5 mitano ya fahamu(Pua -kunusa, sikio- kusikia, ulimi kuonja, Ngozi kuhisi, Macho- kuona) vyote hivyo hupeleka taarifa kwenye Ubongo Kisha Ubongo kutafasiri, hivyo sisi sio binadamu na sisi sio hizo akili(Ubongo) ndio maana tunasema”akili zangu” Yani wewe sio hizo akili, umenipata..?

👉BINADAMU ndani yake amebeba kitu kikubwa kinachompa uhai Kama chaji au BETRI Katika simu kikitoka humo ndani basi Binadamu hana maisha Yani anakufa, kitu hicho kinaitwa ROHO/ENERGY pia ROHO imejikita ndani ya umbo lisiloonekana kwa macho Liitwalo NAFSI(ulimwengu wa Kiroho) hivyo ili twende sambamba jua Roho imo ndani ya Nafsi inaupa uhai nafsi, nafsi Kama kibebeo Cha kwanza Cha Roho pia nafsi nayo imo ndani ya mwili wa kuonekana Yani BINADAMU na viumbe wengine, tupo sawasawa?

NINI HUTOKEA BINADAMU ANAPOKUFA?

👉Sasa Ili kutambua na kujibu swali hilo kiufasaha ni lazima tujue nini hutokea binadamu anapo Zaliwa❓

Ikumbuke Alama ya mti wa Uzima, hapa sizungumzii mti wa uzima wa kufikirika au wa kusadikika unao hubiriwa kwenye Dini za Kikristo na kiislamu, Nazungumzi Mti wa Uzima (Tree of Life) Uliopo ndani yetu kwenye UTI WA MGONGO ambao ukifunguliwa kupitia nishati ya kundalini Huto onja Kifo, ndio lile neno la Fumbo ambalo Yesu wakusadikika anachorwa akimwambia Yohana.

Mk 9:1-25 SUV
Akawaambia, Amin, nawaambia, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapouona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu.

👉Umesikia sasa, hapo Ukiangalia aliyekusudiwa ni Yohana lakini alikufa. Je,lina maanisha nini neno “Hawato onja mauti?” Hapo Yesu wa kusadikika anaechorwa ili kuzungumzia MTI WA UZIMA (TREE OF LIFE) ambao upo ndani ya kila mtu kwenye Uti wa mgongo Wenye tufe za Uhai na Neva pamoja na Nyuzi 12 za DNA (12 DNA Strnds).
Sio kusudio langu kuelezea hiyo habari, Ukiwauliza watu wa mafundisho ya KABBALAH watakueleza vizuri maana ndio msingi wa Mafundisho yao.

👉Ukiitazama alama Ya mti wa uzima inawakilisha chanzo cha Ki-mungu (Energy) cha uhai..au Chanzo cha kiroho cha Uhai.

Ambapo tunazaliwa katika ulimwengu unao onekana na usio onekana.

See also  15 THINGS YOU MUST GIVE YOUR SPOUSE

👉Wachache wanatambua ya kwamba Mti wa Uzima unafanana sana na Tumbo la uzazi la Mwanamke (Placenta).

Ndio maana kwenye Uchawi, Majini, Na nafsi chafu a.k.a Mashetani Hupenda kukaa sana katika tumbo la Uzazi la mwanamke na kizazi chake, Si mnajua hii?….

Tumbo la mwanamke ni mfumo ambao Unalisha, Unatunza na kulinda mwili wa Mtoto ambaye bado hajazaliwa kupitia mrija au kitu kama Kamba kinaitwa UMBILICAL CORD.
Nifupishe nielekee kwenye point ya msingi.

👉Ni kwamba Mtoto ambaye bado hajazaliwa anapo kua ndani ya tumbo la mama yake, anapata chakula na hewa ya Oxygen kumpa uhai kupitia Mrija/Ukamba unaoitwa UMBILICAL CORD unao muunganisha Mama Na mtoto.

Sasa basi Kiumbe kilichopo tumboni.. hufa ..na kiumbe hicho kina ufahamu kwamba kitakufa endapo Ule Mrija/ Umbilical ikikatika na kiumbe hicho kina hofu kama wewe ulivyo na hofu ya Kifo hapo ulipo.

👉Ni kweli Mrija huo unapokatika Kiumbe kina kufa ndani ya Tumbo(Katika ulimwengu wake) lakini pasipo kujua ..kumbe kifo cha kiumbe hicho tumboni ndio Mlango wa Kuzaliwa Upya katika Ulimwengu mwingine ambapo huzaliwa hapa Duniani,

Kwahiyo Kukatika kwa Umbilical cord (kitovu) na kifo cha mtoto tumboni ndio mlango wa kuzaliwa Upya kwenye maisha na uhalisia mwingine. Umenipata? kiukweli Kiumbe Hakifi wala hakuna kufa ila kuna Kuzaliwa katika Ulimwengu mwingine, Kama huu mfano wa Kuzaliwa kwa mtoto.

👉👉Lakini mtoto anapokuwa tumboni humtegemea mama yake kwa kila kitu, kitendo Cha kutoka nje ya njia ya uzazi hapo ndipo ROHO huingia ndani ya huo mwili, Roho isipoingia automatically mtoto anakufa akiwa Katika ulimwengu wa kuonekana ndio maana madaKtari humpigapiga mtoto Hadi akilia hapo huakikisha tayari Roho imeingia na automatically Asili humwelekeza mtoto kunyonya bila kufundishwa..

Ina make sense hapo..?

Tunapata maana ya kwamba Binadamu ni Chombo ama njia ya kuingiza Roho Katika ulimwengu wa kuonekana, hii ndio maana ya Adam na Hawa kula tunda🍎 Yani Sacrade Energy Exchange(SEX) Kisha tunaumba kupitia uzazi kwa kuingiza viumbe vya kimwili na viumbe vya Kiroho duniani, upo hapo?

ROHO hukaa wapi ndani ya Mwili❓

👉Kupitia mfano wa mtoto hapo juu👆 Kwahiyo basi ndani ya kichwa Cha BINADAMU katika Ubongo eneo lenye Tezi inayoitwa penuel(PINEAL GLAND) huitwa JICHO LA TATU(Taa ya mwili) hivyo Kuna mrija au Ukamba usio onekana kwa macho ya nyama na damu kwa Mfano wa Umbilical Cord Mrija huo unaitwa SILVOR CORD una rangi ya dhahabu. Mrija huo kama uonekavyo kwenye picha ni Ukamba unao Tuunganisha Miili hii ya Kifizikia na Roho zetu(sisi) ambazo ndio Uhalisia wetu.

Sisi ni Roho na Roho haifi kamwe ..Hakuna Kufa Roho haifi na Sisi Kiuhalisia ni ROHO sio Mwili. Kwa hiyo SILVOR CORD inaunganisha mwili unaitwa binadamu na Roho ambazo ni sisi viumbe wa kiroho

Nini kinatokea baada ya Roho kuuacha mwili?

Awali kabisa nilisema Roho ambayo ni nishati haifi Bali hujibadili badili kutokana na mazingira tofauti tofauti. Katika maandiko ya nyuma niliwahi KUFUNDISHA kuhusu kitu kiitwacho KARMA(the law of cause and effects) Yani sheria ya Chanzo na madhara, Yani unavuna ulichokipanda(what goes around comes around)

👉Pia tunafahamu ya kuwa Mungu/Roho/Nishati ni UFAHAMU/CONSCIOUSNESS na Ufahamu huu upo Katika Asili (vitu) mbalimbali na kila kitu kina kiwango chake Cha Ufahamu mfano:-

  1. Mineral kingdom
  2. Plant kingdom
  3. Animal kingdom
  4. Human kingdom

👉Ufahamu uliomo ndani ya mawe, ardhi upo chini kuzidi Ufahamu ndani ya mimea, na mimea inaufahamu mdogo kuzidi Wanyama na wanyama wapo chini kiufahamu kuzidi BINADAMU ijapokuwa hizo kingdom zote Nazo zinatofautiana kiufahamu kwani Ufahamu wa sokwe ni wa juu kumzidi Mbwa ama Ufahamu wa mtu anayejitambua ni tofauti na Ufahamu wa mtu aasiyejitambua habadani.

See also  JE KAZI ZA KIBAILOJIA ZA GOVI NI ZIPI NA NINI HUTOKEA LINAPOONDOLEWA?

👉Kutokana na Roho kunyumbuka kwa kujiweka(kuji-stole) Katika Asili , hutegemea Asili hiyo ama kitu hicho wakati kinakufa KILIKUWA Katika kiwangogani Cha Ufahamu , Sasa tukija kwa kiumbe aitwaye BINADAMU anayo nafasi pekee ya kukuza Ufahamu wake kuzidi kiumbe chochote Katika hii Dunia, hivyo Ufahamu wake hutokana na matendo yake ama tabia yake mfano BINADAMU aliyekufa akiwa ana tabia za unyama mfano kuua , kujeruhi ama kuumiza VIKALI watu wengine ama viumbe wengine maana yake BINADAMU huyo alishusha ufahamu wake kutoka Ufahamu wa MTU (human kingdom) Hadi Ufahamu wa Wanyama(Animal kingdom) mithili ya Simba, chui , Mbwa n. K

Kutokana na Asili kufuata kanuni za Creation/ Uumbaji ,Roho ya binadamu wenye tabia za mnyama ataingia na Kuzaliwa Katika jamii ya Wanyama , hivyohivyo mwenye tabia za wadudu ataingia/atazaliwa Kwenye wadudu n. K

👉Ile maana ya kuvuna ulichokipanda Yani KARMA ni kupokea matokeo yale yale ya nguvu ileile uliyoituma ama kuitoa, kwa mantiki hii Binadaku akifa akiwa Katika tabia nzuri alizoziishi mfano kusaidia watu, huruma, upendo basi MTU huyo angali amekufa akiwa Katika Ufahamu uleule wa kibinadamu atazaliwa Tena kwa kuingia ndani ya kichanga Cha mama anayejifungua Katika jamii ya Binadamu EIDHA ndani ya ukoo ule ama nje ya Koo yake, nchi yake, ama Kuzaliwa Katika sayari ingine yenye viumbe (watu) wengine wenye Ufahamu wa juu zaidi Kama marehemu kabla ya kifo alikuwa Katika level ya juu ya Ukiroho/Ufahamu n. K

Wewe tangu uzaliwe Hadi Leo huwazi lolote zaidi ya kula bata, ilimradi hulali njaa Huna hata wazo la kujenga kibanda Yani umekuwa teja , Yani wewe huna tofauti na kuku kutwa kupekua msosi hakika umekuwa na tabia za ndege basi si ajabu kuingia ukazaliwa Kama kunguru.

👉Ijapokuwa sisi Roho tupo katika Mtego tuliojiwekea(Asili ilivyojiseti) kwa kujiingiza Katika viumbe wa kimwili ili kukuza Ufahamu wetu na Uzoefu ili kurudi Katika ule ukuu wetu ambao kupitia mwili tukifikia hatua ya 7 ya Ufahamu na tukawa Mungu mtu Yani ukatawala ulimwengu wa nje na wa ndani(usioonekana na unaoonekana) Kwa pamoja tunasema wewe umetamalaki, umejitambua(enlightened) kwa hakika wewe ukiukacha mwili hutorudi Kuzaliwa Katika mwili kwakuwa utakuwa umemaliza lile kusudio la kuingia katika mwili, utapaa Kama Yesu wakusadikika alivyopaa ikiwa ni lugha ya kificho kuwakilisha chakra ya 7 Yani taji la kichwa(chrown chakra) Yani KITI CHA ENZI.

Note👉Hakuna KUFA Bali ni kuhama(shifting) kutoka Katika Dimension/ulimwengu mmoja kwenda Mwingine hasa ulimwengu wa Kiroho, kila kiumbe ukionacho Duniani kwakuwa ndani yake Kuna Roho Yani ule Ufahamu(consciousness) basi kitu hicho kinahamia Katika ulimwengu wa Kiroho wa kwanza ambako kupo Kama uonavyo hii Dunia Ila utofauti huko kila kiumbe kipo Katika kupambana kurudi Duniani Kwa KUONGEZA Ufahamu wake, Miti, mimea, wanyama, ndege, watu (nafsi zote hizo) viumbe vyote hivyo hupanga foleni kurudi Duniani ijapokuwa hii hatua huchukua muda kuanzia miaka 3/4 Hadi miaka 500/600 ambapo Katika ulimwengu wa Kiroho mwaka mmoja ni sawa na siku 3/5 duniani na iyo miaka 600 Kiroho ni sawa na miaka 4-5.
👉Kama Kuna ndugu yako aliyewahi kuchanganyikiwa Kisha kupona ukimuhoji Kama alitumia siku 30 kupona Yani kurudi Katika Hali yake ya awali, ukimuhoji kule Katika ulimwengu wa Kiroho alitumia muda gani anaweza kukwambia ni sawa na masaa 6 tu ,Yani kumbukumbu yake itakumbuka kuwa niliugua Leo saa 2 asubuhi naamini ilipofika saa 8 mchana ndio nimerudi,wakati ninyi mliomuuguza mna hesabu ni siku ya 30(mwezi😁) iko hivi- mtu akichanganyikiwa Huwa kiwiliwili yupo Duniani muda huohuo yupo ulimwengu wa Kiroho ndio maana unaweza muona anaongea, anacheka peke yake ukadhani nimukichaa Ila ukweli anaona watu(nafsi) na anaongea nao yupo anakula maisha Kama kawaida.

Wazee (ancestors) wetu Ufahamu huu waliweza kuujua kutokana na uwezo wao wa juu Kiroho na kuweza KUFUNGUA mipaka kwa kuona namna viumbe wa kiroho vinavyoshift kutoka sehemu moja kuingia ulimwengu Mwingine, kwa wewe na Mimi IPO njia kuu ambayo ni kushiriki meditation itakufundisha kila kitu hata niyasemayo ni punje ya mchanga ndani ya pipa la maji, yapo mengi hayaelezeki ndio lile fumbo la yeremia33:3-Niite nami nitaitika nitakuonesha Mambo magumu usiyoyajua…..)

See also  MIAKA MITATU BILA JOHN POMBE MAGUFULI KESHO

👉Nihitimishe kwa kusema hatupo hapa kutafuta familia, Mali, ufahari, umaarufu, Bali tupo hapa kufungua mipaka, Mtego (matrix) ilikufungua malango Nyota (star gets) ili turudi Katika ukuu wetu UHALISIA wetu, lakini kufa na Kuzaliwa Tena ni mzunguko(Mtego/fumbo/matrix) utakaoendelea kwa jamii yote isiyoweza kuufikia Ufahamu wake wa juu(umungu) hivyo utaendelea Kuzaliwa Hadi pale utakapojitambua wewe ni Nani, upo hapa kwa lengo gani na Nini hatima ya wewe kuwa hapa Duniani, usipojitambua utaendelea kutumwa na wazee wako nafsi zilizokufa zamani Katika ule ulimwengu wa Kiroho Yaani 4D ambao huuona kupitia njozi zetu Nzuri kinachofanyika wazee(miungu yako ya ukoo) inakutuma(ule wimbo wa “nimtume nani” ) ili uzaliwe Tena hapa duniani for special purpose ambayo ni Ile Nyota yako(ijue Nyota yako)hivyo unatakiwa utoke ndani ya Mtego huu ili kuweza kupaa(kuishi maisha yetu ya Asili ya hapo awali kabla ya mipaka -ulinwengu wa 3D)

👉Katika Ubongo🧠 wa mwanadamu Kuna eneo huitwa HIPPOCAMPUS eneo hili hutunza kumbukumbu inazozipokea, Sasa Kwa mtu Anayefanya meditation eneo hili hufuta kabisa kumbukumbu zote ovu/mbaya Kwa kadri unavyozidi kuexperience meditation basi eneo Hilo huhifadhi/kureplace yake matukio mazuri , kwa maana hiyo Mtu anayeshiriki mara kwa mara meditation Huwa mwenye tabia Njema hatokuwa na tamaa, Wivu, Uongo, wizi, Roho ya ukatili Kwasababu Brain yake haijui kuwa Kuna hizo tabia, unaweza mtukana mtu wa namna hii leo Kisha kesho ukakutananaye akakukumbatia Kwasababu Hana kumbukumbu ya matendo uliyomfanyia Jana, hii ndio Siri ya marasi wengi (Rastafar) kupendwa na Wazungu kwani maras japo sio wote hufanya meditation lakini marastar wengi wanapata elimu ya Ukiroho hivyo mzungu ana uhakika camera yake, laptop yake fedha zake,simu yake ziko sehemu salama kwenye mizunguko yao ya kitalii n.k

💊Ondokana na Uongo na Vitisho vya Kidini kuwa ipo siku utakufa Kisha utaenda kizimbani kuhukumiwa na Mungu ili uingie motoni🔥 ama peponi, ukweli unatakiwa Ufahamu kuwa jehanam, motoni , peponi ni hapa hapa Duniani unapata kile unachokitaka kutegemeana na matendo yako, Sasa Kama umetambua kuwa hakuna kifo basi yawezekana hiyo misukosuko uliyonayo ni matokeo ya Karma Yani Asili imekurudisha katika huo mwili ili ulipe Makosa yako uliyoyatenda Katika mwili wa zamani hivyo ukimlilia bwana Yesu ama sijui Allah nikujipotezea muda tu, unachotakiwa Kujua ni kuwa kila kinachokutokea umekizalisha mwenyewe,hivyo kwa Sasa yafaa kuanza maisha upya pata elimu ya Kiroho Kama hii ninayokushushia uishibe haswa ili uyaishi maisha ya Asili maisha ya Upendo ili upokee matokeo Chanya yasiyoumiza Bali yakufurahishayo ili uenjoy kuwa mmoja wapo wa wavunaji wa hii Dunia.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

UTAMU WA MECHI YA AZAM NA YANGA...
MICHEZO Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara inaendelea tena leo...
Read more
10 SIGNS OF A TRUE GIRLFRIEND 💌🤝💐🌹
True girlfriends are very jealous. If you are dating them,...
Read more
A DIFFERENCE BETWEEN A COMPANY PROFILE &...
BUSINESS PLAN A business plan is a written document that outlines...
Read more
16 IMPORTANT THINGS COUPLES SADLY STOP DOING...
LOVE ❤ 1. SAYING I LOVE YOU It is sad...
Read more
TUNDU LISSU AMSHTUKIA MBOWE KUELEKEA 2025
HABARI KUU Baada ya Lissu kutangaza jukwaani kuwa rushwa imekithiri...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply