CODY GAKPO ASIMULIA FURAHA YAKE KUWA NDANI YA LIVERPOOL

0:00

MICHEZO

Mshambuliaji kutoka nchini Uholanzi Cody Gakpo amefichua kuwa alifanya mazungumzo na Manchester United kuhusu uhamisho wa msimu wa majira ya joto wa 2022, lakini kuhamia kwake Liverpool msimu wa baridi mwaka uliofuata kwa kusema ulikuwa uamuzi bora kwake.

Mshambuliaji huyo mwenye uwezo mwingi alifurahia miaka mitano katika kikosi cha kwanza cha PSV Eindhoven kabla ya kusajiliwa na wekundu hao Januari 2023.

Wakati wa Erik ten Hag akianza kuinoa United, Gakpo alifanya mazungumzo naye kuhusu kuhamia Old Trafford, lakini hatimaye makubaliano hayakuweza kukamilika.

Gakpo alibaki PSV hadi dirisha la majira ya baridi na kisha akajiunga na Liverpool kwa dau la awali la Pauni Milioni 35.4.

Katika mahojiano na Sky Sports, Gakpo alifunguka juu ya ukubwa wa mazungumzo haya ya uhamisho na Man Utd na jinsi ilivyokuwa bora kwake kubaki na kusubiri kutua Liverpool.

“Tulikuwa majira ya joto kabla ya kujiunga na Liverpool. Nilikuwa nikiwasiliana na klabu (United) na kocha yeye ni Mholanzi kwa hivyo nilizungumza naye pia,” alisema Gakpo.

“Mwisho wa siku ilishindikana, na wakati wa majira ya baridi Liverpool ilikuja. Ulikuwa uamuzi bora kwangu.”

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

HISTORIA YA MAISHA YA MSANII BEN POL...
NYOTA WETU Alianza kuimba tangu akiwa shule wakati anasoma sekondani...
Read more
YANGA YAWASILISHA MALALAMIKO HAYA CAF
MICHEZO Klabu ya Yanga imewasilisha malalamiko kwenda CAF kuhusu uwezekano...
Read more
Klabu ambazo Ziko Mbioni Kununua Mkataba wa...
Story zinazotrend Nchini ni : ◉ Aziz Ki kuhusu mkataba mpya...
Read more
HAJI MANARA AZIDISHA MOTO SUALA LA PRINCE...
MICHEZO
See also  Mfahamu Mrithi wa Ugombea Urais wa Marekani Baada ya Joe Biden Kujiondoa?
Baada ya Mchambuzi wa masuala ya kandanda Jemedari Saidi...
Read more
Jinsi Israel Inavyoweza Kuwauwa Viongozi Wakuu wa...
Ujasusi Wa Israel Ndani Ya Ardhi Ya Iran… Ismael Haniyah anazikwa...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply