0:00
HABARI KUU
Watendaji Wakuu wa Mtandao wa X (zamani Twitter) ambao walifukuzwa kazi baada ya Elon Musk kuununua Mtandao huo, wamefungua Kesi ya madai wakimtaka Bosi huyo mpya kuwalipa zaidi ya Tsh. Bilioni 326 kwa kuwaondoa kazini kikatili.
Kesi hiyo imefunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya San Francisco walalamikaji wakiwa ni aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Twitter, Parag Agrawal pamoja na Watendaji wengine watatu wanaodai Elon alivunja haki za Wafanyakazi waliofukuzwa baada ya kuinunua kampuni hiyo.
Taarifa zaidi zinadai hadi kufikia Mwaka 2021, Agrawal alikuwa na madai ya fidia yenye thamani ya zaidi ya takriban Tsh. Bilioni 76.5 kutoka katika kampuni hiyo.
Related Posts 📫
Amethyst ni moja kati ya vito vya thamani vinavyojulikana kama...
LOVE ❤
1. Relax. Know that tough times and challenges...
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limemtoza faini ya Dola...