AFYA YA PAPA FRANCIS YAZIDI KUZOROTA

0:00

NYOTA WETU

Kwa mara nyingine tena Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis, alimuomba Msaidizi wake kumsomea somo la katekisimu wakati wa misa ya Jumatano.

Papa aliongoza misa hiyo ya kila wiki ambayo kwa mara ya kwanza ndani ya mwaka huu ilifanyikia nje katika uwanja wa St.Peters.

Kiongozi huyo pia alionekana kushindwa kupanda ngazi chache na kutoweza kurudi kwenye gari lake maalumu bila msaada kwani bado matatizo ya mfumo wa upumuaji na shida ya kutembea vinaendelea kumsumbua.

Jumatano iliyopita, Papa Francis alipelekwa hospitali kwa vipimo ambavyo havikutajwa na hadi sasa matokeo ya vipimo hivyo hayajawekwa wazi.

Katika kipindi hiki cha baridi barani Ulaya Papa amekuwa akiugua mara kwa mara kwa kile ambacho yeye mwenyewe pamoja na Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Vatican imekitaja kuwa ni kikohozi, mafua na shida kwenye mfumo wa upumuaji.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

GABRIEL AMPIGIA CHAPUO SALIBA
MICHEZO Beki kutoka nchini Brazil na Klabu ya Arsenal Gabriel...
Read more
Mwili wa Ebrahim Raisi wapatikana
BREAKING NEWS Mwili wa aliyekuwa Rais wa Iran, Ebrahim Raisi...
Read more
Netizens drag Helen Paul for saying "women's...
Comedian and actress, Helen Paul, has attracted backlash after suggesting...
Read more
Police Nominee Vows to Fortify Parliament, Pledges...
In his testimony before the National Assembly Committee on Administration...
Read more
TAKWIMU ZA FEISAL SALUM NA STEPHAN AZIZ...
MICHEZO Nani ataongeza goli leo katika kinyang'anyiro cha ufungaji ?Hizi...
Read more

Leave a Reply