WATU 50 WAJERUHIWA KWENYE NDEGE NEW ZEALAND

0

0:00

HABARI KUU

Takribani watu 50 wamejeruhiwa baada ya Ndege iliyokuwa ikisafiri kutokea Sydney,Australia kuelekea Auckland, New Zealand kupatwa na hitilafu ya kiufundi ikiwa hewani.

Taarifa iliyotolewa na Shirika la Ndege la Chile (LATAM) imeeleza kuwa Ndege hiyo aina ya Boeing 787-9 Dreamliner ilipatwa na hitilafu iliyosababisha kusonga kwa nguvu kubwa.

Tukio hiko lilisababisha abiria saba na wahudumu watatu wa Ndege hiyo kupelekwa hospitali mara tu baada ya kutua, huku wengine takribani 50 wakipatiwa huduma ya kwanza kwa majeraha.

Magari saba ya wagonjwa, Magari mawili ya dharura na mengine mawili ya kutoa sapoti wakati wa maafa yalifika uwanjani ili kuingojea ndege hiyo tayari kwa kutoa huduma stahiki kwa walioathirika.

Shirika hilo la Ndege limeeleza kusikitishwa kwake na matokeo yote ya hitilafu hiyo, huku likisisitiza kuwa siku zote usalama wa wasafiri ndicho kipaumbele chao.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  REASONS HUSBANDS LEAVE THEIR WIVES FOR ANOTHER WOMAN
Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading