AFA BAADA YA KUWAPA WANAE SUMU

0:00

HABARI KUU

Mkazi wa Kijiji cha Mashese, Daines Paul Mwashambo (30),  ambaye alikuwa akishikiliwa kwa tuhuma za kuwaua watoto wake wawili kwa kuwanywesha sumu kutokana na msongo wa mawazo amefariki dunia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema Daines alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya na alifariki dunia Machi 9, 2024 majira ya saa 10:15 jioni.

Amesema, marehemu akiwa nyumbani kwake Kijiji cha Mashese – Ilungu aliwanywesha sumu ya kuulia magugu aina ya ‘Pare Force’ watoto wake wawili na kusababisha vifo vyao na kisha na yeye alikunywa sumu hiyo ya kuulia magugu iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya kwa matibabu.

Kamanda Kusaga amewataja watoto hao waliofariki muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya kwa matibab kuwa ni Mario Semen Adamson (4) na mdogo wake wa kike Beonis Semen Adamson (2), wote wakazi wa Mashese.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Mbwana Samatta aisaidia PAOK kubeba Ubingwa
MICHEZO Nahodha wa kikosi cha Timu ya Taifa Tanzania (Taifa...
Read more
ADIDAS YAMPA MESSI ZAWADI HII ...
NYOTA WETU Lionel Messi azawadiwa Pete nane za dhahabu kuwakilisha...
Read more
KURASA ZA MAGAZETI YA LEO YA TANZANIA
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
BURUNDI NA TANZANIA KUFANYA BIASHARA YA PAMOJA
HABARI KUU SERIKALI kupitia Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) imetia...
Read more
The Supreme Court has dismissed an application...
Ajaka had urged the apex court to await the outcome...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply