MICHEZO
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema Nahodha wa Timu ya Taifa Mbwana Samatta hajaitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa sababu alimuomba Kocha Hemed Suleiman asimjumuishwe kwenye kikosi hiko kuelekea michezo ya FIFA Series.
“Nahodha wa Timu ya Taifa Taifa Stars, Mbwana Samatta ameomba kutojumuishwa kwenye kikosi kilichoitwa kwa michezo ya FIFA Series 2024, amezungumza na Kocha kabla ya kutajwa kwa kikosi hicho na kuomba asijumuishwe katika
safari hiyo ya Azerbaijan, ombi ambalo limekubaliwa”
“Kikosi hicho kitakachoingia kambini Machi 17, 2024 kitaondoka Machi 18, 2024 na kitacheza michezo miwili na Bulgaria na Mongolia, michezo itayochezwa Machi 22 na Machi 25, 2024 Kikosi kinatarajia kurudi Machi 27, 2024”
Taifa Stars itandoka nchini kuelekea Azerbaijan kwa ajili ya michezo ya FIFA Series ambapo huo ni utaratibu mpya uliyoanzishwa na FIFA.