WATU 9 WAFARIKI BAADA YA GARI LAO KUSOMBWA NA MAJI

0:00

HABARI KUU

Watu tisa wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noah lenye namba za usajiri T795 BIS kusombwa na maji kwenye mto Kisimani katika Kijiji cha Lumeme kilichopo Halmashauri ya Nyasa Mkoani Ruvuma.

Akithibitisha kutokea kwa tulio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya amesema tukio hilo limetokea Machi 11, 2024 baada ya gari hilo kusombwa na maji.

Amesema, chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva ambaye alilazimisha kuvuka wakati Mto huo ukiwa umejaa maji, na kutoa rai kwa Madereva na Wananchi kuacha tabia ya kupima maji katika madaraja kwa kuyatazama.

Amewataja waliofariki kuwa ni Edwini Abeli Ngowoko (55), Matengo (Dereva wa Gari), Valeliana Ndunguru (18), Innocent Cassian Ndunguru ( 63), Simon Mahai (21) na Nathan Kumburu (39).”

“Wengine ni Faraja Daud Tegete (18) ambaye ni Mwanafunzi wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari Kilumba, Ebiati Daud Tegete (2) na Alfonsia Casian Mbele (40).

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

SABABU ZA BAKARI MWAMUNYETO KUGOMEA KURUDI YANGA
NYOTA WETU Nahodha wa timu ya Yanga amegoma kurejea kambini...
Read more
Aliyekuwa mgombea wa kanda ya Nyasa ya...
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Juni 3, 2024...
Read more
BURUNDI NA CONGO ZAUNGANA KUIPIGA RWANDA
HABARI KUU. Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye amesema atawasaidia vijana...
Read more
"Envy exist in almost every extended family...
OUR STAR 🌟 Controversial Nollywood actor, Yul Edochie has taken...
Read more
Former Aviation Minister, Femi Fani-Kayode, has asserted...
Biden made the endorsement shortly after he announced that he...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  MANCHESTER CITY YAICHAPA MANCHESTER UNITED

Leave a Reply