Mkuu wa Wilaya Morogoro Rebeca Nsemwa ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu Diwani Kata Mwembesongo Mhe.Ally Rashidi Kalungwana Kwa kitendo cha Kutumia vibaya madaraka yake kujenga vibanda vya biashara katika eneo la wazi Soko Kuu la chifu Kingalu Manispaa ya Morogoro

0:00

DC Rebbeca amesema Diwani huyo amejenga vibanda vya kufanyia biashara katika Soko Kuu la Chifu Kingalu bila kufuata taratibu za mipango miji jambo ambalo ni kosa kisheria na kutaka achukuliwe hatua za kinidhamu haraka sana Ili iwe fundisho kwa watu wengine.

DC Rebbeca anasema licha ya Diwani huyo kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya mipango miji Halmashauri Manispaa ya Morogoro, lakini amekua mtu wa kwanza kuvunja sheria hivyo lazima awe mfano kwa watu wanaotumia madaraka yao vibaya.

Mwenyekiti wa soko Hilo la Chifu Kingalu, Khalid Mkunyegele anasema licha ya uongozi wa soko kumkataza kujenga lakini alikaidi amri hiyo na kuendelea hadi kamati ya usalama Wilaya ilipofika na kubomoa vibanda hivyo ambayo vimejengwa pembeni ya soko kuu .

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

"I WAS BORN FOR PEOPLE TO LOOK...
OUR STAR 🌟 Popular reality star, Doyin brags about her...
Read more
SABABU DANI ALVES KUACHIWA HURU
MICHEZO Mahakama ya Hispania imesema mlinzi wa zamani wa FC...
Read more
CHADEMA YAMTOSA MATIKO UBUNGE TARIME MJINI
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
MORGAN FREEMAN AFICHUA SIRI YA KUVAA HERENI...
NYOTA WETU. Muigizaji wa filamu Morgan Freeman afichua siri za kuvaa...
Read more
WOTE NI MINNE TENA! Wape Kura siyo...
Jumapilli 14/7/2024 dunia ilitaharuki kusikia huko Marekani, mgombea urais wa...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  WASANII WA KIKE WA TANZANIA WANANYANYASWA KINGONO

Leave a Reply