SABABU ZA MGOMO WA MADAKTARI KENYA

0:00

HABARI KUU

Mgomo wa madaktari katika Hospitali za Umma kote Nchini Kenya, umeanza rasmi hii leo Machi 14, 2024, huku baadhi ya jamaa wakilazimika kuwaondoa wagonjwa wao katika Hospitali hizo, ili kutafuta huduma za matibabu kwingine.

Hata hivyo, shughuli za kawaida katika Hospitali kuu ya Rufaa na Mafunzo ya Kilifi zimeendelea, hivyo kukinzana na tamko la Muungano wa Madaktari ukanda wa Pwani – KMPDU, la mgomo wa Madaktari.

Mmoja wa wauguzi aliyeongea kwa sharti la kutotaja jina, amesema wanaendelea na kazi ya kuhudumia wagonjwa kama kawaida, baada ya uongozi wa madaktari Kilifi kufanya mkutano na Serikali ya Kaunti ya Kilifi.

Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno nchini Kenya – KPMDU, ulitangaza mgomo wakiishinikiza Serikali kutimiza mahitaji yao muhimu, ikiwemo kurejeshwa kwa makato ya ushuru wa Nyumba yaliyofanyika katika mishahara yao, ambayo Mahakama ilitangaza kuwa yanafanyika kinyume na Katiba.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

NDOTO YA KOCHA SVEN-GORAN ERIKSSON YATIMIA AKIWA...
NYOTA WETU Meneja wa zamani wa timu ya Taifa ya...
Read more
JOSEPH MBILINYI "SUGU" AMBWAGA PETER MSIGWA
Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu Sugu...
Read more
Aston villa leave it late in 3-1...
Aston Villa denied Wolverhampton Wanderers their first victory in the...
Read more
Kwanini Jurgen Klopp amekataa Kuiongoza Marekani kama...
Aliyekuwa kocha wa Liverpool ametupilia mbali ofa ya kurejea mzigoni...
Read more
JONAS MKUDE AMSHTAKI MO DEWJI ...
NYOTA WETU Mchezaji wa klabu ya Yanga, Jonas Mkude amefungua kesi...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  TIPS FOR MEN ON HOW TO APPROACH A WOMAN

Leave a Reply