Droo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imekamilika huku vigogo 8 waliofuzu hatua hiyo wakibaini wapinzani wao.
Kama kawaida, Washika Mitutu, Arsenal wamepangwa dhidi ya Bayern Munich kwenye hatua hiyo huku Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo, Manchester City wakikutanishwa na Mabingwa wa kihistoria, Real Madrid.
Barcelona imepewa PSG huku Atletico Madrid ikipewa Borussia Dortmund.
DROO KAMILI
Arsenal vs. Bayern Munich Atletico Madrid vs. Dortmund Real Madrid vs. Manchester City Paris Saint-Germain vs. Barcelona
Mshindi kati ya Arsenal na Bayern Munich atachuana na mshindi kati ya Real Madrid na Manchester City kwenye hatua ya nusu fainali.
Mshindi kati ya PSG na Barcelona atachuana na mshindi kati ya Atletico Madrid dhidi ya Borussia Dortmund.