Salah amekuwa na mchango mkubwa kwa Liverpool tangu ajiunge nayo mwaka 2017 akiisaidia kushinda Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa, Carabao na FA Cup.
Msimu huu Liverpool inashiriki michuano ya Europa ikiwa ni baada ya kushindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa msimu uliopita na mara nyingi kwenye michuano hii wameonekana kutumia wachezaji vijana kutoka kwenye akademni yao.
Inaelezwa kwamba Salah ndio amekuwa akiwasimamia wachezaji hao na kuongea nao mara tu wanapokuwa wanapandishwa kwenye kikosi cha kwanza tofauti na ilivyodhaniwa kwamba, jamaa anaringa na hapendi wenzake wafanikiwe.
“Kitu kikubwa ambacho nakifanya ni kuzungumza nao, na kuonyesha kwamba unawajali kabla hata ya kuwapa ushauri wowote, kama ukiwapa tu ushauri bila ya kuwaonyesha kama unawajali wanaweza wasisikilize ushauri wako.
“Lakini kama utamuonyesha kumjali na kumwambia kwamba ataenda kufanya mambo makubwa na ataonyesha kiwango bora na akienda uwanjani afanye tu vitu vidogo ili kubadilika siku hadi siku, mimi kila siku nawaonvesha kwamba nawajali kisha baada ya hapo inakuwa rahisi kuongea nao na kuwaweka mkononi.”
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.