Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete ametunukiwa tuzo ya kiongozi bora wa mwaka 2023 katika Tuzo za Kiongozi Bora wa Afrika kwa Mwaka 2023 (African Leadership Person of the Year) kama Kiongozi Bora wa Mwaka katika Amani na Usalama barani Afrika.

0:00

Katika hotuba ya Dkt. Kikwete wakati wa hafla hiyo iliyoandaliwa na Jarida la Uongozi Afrika (ALM) jijini Addis Ababa, Ethiopia ameshukuru kwa kutunukiwa tuzo hiyo na kuwasihi Waafrika wote kwenye nafasi za uongozi kutoa kipaumbele kwenye masuala kutatua changamoto zilizopo ikiwemo umasikini, changamoto ya chakula, mabadiliko ya tabia ya nchi, magonjwa, ujinga, migogoro ya kisiasa na vita.

“Ukweli ni kwamba, ni kwa heshima kubwa ninakubali kupokea tuzo hii. Naipokea,
si tu kwa ajili yangu bali kwa niaba ya Waafrika wengine wengi; wawe viongozi wa kisiasa, wenye ushawishi kiuchumi, viongozi wa dini, wanachama wa vikosi vya usalama, watumishi wa umma, na wananchi wa kawaida ambao huamka kila siku na kufanya sehemu yao katika kulifanya Bara la Afrika kuwa sehemu nzuri zaidi ya kuishi,” amesema Dkt. Kikwete.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

KANUNI 14 ZINAZOWEZA KUKUONGOZA KWENYE MAHUSIANO ...
MAPENZI. Mwongozo ni kama katiba ilivyo ambako kanuni na sheria...
Read more
SABABU ZA KIFO CHA MWANAHARAKATI ANNE RWIGARA...
HABARI KUU. Mkosoaji wa Serikali ya Kigali wa muda mrefu,...
Read more
Vee and Magixx from BBNaija set tongues...
Social media has been inundated with reactions following the unveiling...
Read more
MANCHESTER UNITED have reportedly agreed personal terms...
Erik ten Hag is desperate to add a defensive midfielder...
Read more
Mbappe should score more ,says Carlo Ancelotti
Real Madrid forward Kylian Mbappe should prioritise scoring over pressing...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  SNOOPDOG ATANGAZA KUACHA KUVUTA BANGI

Leave a Reply