CHAKULA CHA WAMAREKANI KIKO SALAMA YASEMA TBS

0:00

HABARI KUU

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesema msaada wa chakula uliotolewa na wizara ya Kilimo ya Marekani kwa ushirikiano na Taasisi za Jumuiya ya Kimataifa katika baadhi ya shule za mkoa wa Dodoma ulifuata taratibu za uingizwaji wa chakula nchini.

Taarifa ya TBS iliyotolewa kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa chakula hicho kilipoingizwa nchini kilifanyiwa ukaguzi na uchunguzi wa kimaabara na kuthibitishwa kuwa ni salama kwa matumizi.

TBS imetoa taarifa hiyo kufuatia taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na msaada wa mchele ulioongezwa virutubishi, mafuta ya kupikia yaliyoongezwa virutubishi na maharage vilivyotolewa na taasisi hizo za nchini Marekani kupitia mpango wa Pamoja Tuwalishe.

Aidha, TBS imesisitiza kuwa utaratibu wa kuongeza virutubishi kwenye chakula unakubalika kitaalamu na hufanyika kwa lengo la kuboresha hali ya lishe kwa walaji.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Mmiliki tajiri wa vyombo vya habari duniani,...
Murdoch mwenye umri wa miaka 93 amefunga ndoa hiyo jana...
Read more
Kurasa za Magazeti ya leo
Read more
MWANAMZIKI WA FM ACADEMIA AFIA JUKWAANI ...
NYOTA WETU Mwanamuziki nyota wa FM Academia, Malu Stonch amefariki...
Read more
SUALA LA THABO MBEKI LILIVYO KWASASA
HABARI KUU Taasisi ya Thabo Mbeki imepinga vikali tetesi zilizovuma...
Read more
NIGERIA COMEDIAN AYO MAKUN HUMOROUSLY DRAGS HIS...
OUR STAR 🌟 “You refused to do same for me”...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Mkuu wa Wilaya Morogoro Rebeca Nsemwa ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu Diwani Kata Mwembesongo Mhe.Ally Rashidi Kalungwana Kwa kitendo cha Kutumia vibaya madaraka yake kujenga vibanda vya biashara katika eneo la wazi Soko Kuu la chifu Kingalu Manispaa ya Morogoro

Leave a Reply