KESI YA PAULINE GEKUL BADO MBICHI

0:00

HABARI KUU

Mahakama Kuu Kanda ya Manyara, imepanga kusikiliza rufaa ya tuhuma ya kushambuliwa kwa kijana Hashimu Ally na Mbunge wa Babati Mjini (CCM), Pauline Gekul, machi 21,2024.

Jaji wa Mahakama hiyo, Devotha Kamzora ameyasema hayo wakati akisikiliza hoja za wawawakilishi wa upande wa Hashimu na Gekul, akisema taarifa zilizowasilishwa hazina sifa ya kuendelea kwa shauri hilo, kwa mujibu wa kifungu cha Sheria namba 190 chenye wajibu wa Mahakama kutoa wito kwa mshtakiwa.

Jopo la Mawakili watatu upande wa mlalanikaji, likiongozwa na Wakili Peter Madeleka limebainisha kwamba litahakikisha haki ya mteja wao inapatikana kwa Mahakama kutimiza wajibu wake katika misingi ya haki.

Kwa upande wa Mbuge Gekul, umewakilishwa na Mawakili wawili wakiongozwa na Efraimu Kisanga ambao wamesema awali hawakuona nyaraka za wito wa Mahakama, kitendo ambacho kinatoa fursa kwenda kupitia maombi ya walalamikaji kabla ya kuanza kusikilizwa.

Pauline Gekul

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress (ANC), kina kila dalili za kupoteza wingi wa wabunge kwa mara ya kwanza tangu kilipoingia madarakani miaka 30 iliyopita. Huku asilimia 50 ya kura zikiwa tayari zimehesabiwa, ANC inaongoza kwa asilikia 42, ikifuatiwa na Democratic Alliance (DA) yenye asilimia 23.
Don't miss out!
Invalid email address

By Mujuni Henry

JUNIITV

Please disable your adblocker or whitelist this site!

         banner                            

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading