MICHEZO
Mcheza tennis namba mbili kwa ubora Duniani upande wa wanaume mhispania Carlos Alcaraz ameshinda ubingwa wa michuano ya Indian Wells 2024 na kutetea ubingwa wa michuano hii, baada ya kumfunga mrusi Daniil Medvedev kwenye mchezo wa fainali kwa seti mbili 7-6 na 6-1 mchezo uliochezwa California Marekani.
Baada ya ushidni huu Alcaraz alielezea furaha yake kwa kutwaa ubingwa kwa mwaka wa pili mfuulizo.
“Najisikia vizuri kwa sasa, mashindano haya yana maana kubwa kwangu, kucheza hapa ni jambo la kipekee sana kwangu, lakini nadhani mwaka huu ni wa kipekee zaidi kwa sababu kabla ya michuano hii nilikuwa nafikiria kama naweza kucheza kwa ubora wangu au la.’’ Alisema Alcaraz
Alcaraz mwenye umri wa miaka 20 amekuwa mchezaji wa kwanza kushinda ubingwa wa Indian Wells mara mbili mfululizo tangu mwaka 2016 aliposhinda Novak Djokovic, pia Carlos Alcaraz amekuwa mchezaji wa 6 kushinda michuano hii miaka miwili mfululizo.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.