GABRIEL MAGALHAES APATA MAJERAHA TIMU YA TAIFA YA BRAZIL

0:00

MICHEZO

Arsenal imetikiswa baada ya beki wake mahiri kabisa, Gabriel kujiondoa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil baada ya kudaiwa anasumbuliwa na maumivu.

Beki huyo wa kati alitarajia kuanza kwenye mechi ya Jumamosi (Machi 23) dhidi ya England itakayopigwa huko Wembley akiwa na kikosi cha Brazil maarufu kama Samba Boys.

Hata hivyo, alifanya mazoezi kidogo kwenye kambi ya timu ya taifa ya Brazil iliyopo kwenye viwanja vya mazoezi ya Arsenal, London Colney, lakini aliondolewa kwa kikosi ili asiumie zaidi baada ya kuonekana kuwa na tatizo.

Maumivu hayo mapya hayahusiani na yale ya mguu ambayo yamekuwa yakimsumbua Gabriel kwa siku za karibuni.
Kocha wa Brazil, Dorival Junior alisema beki huyo ameondolewa kwenye kikosi cha nafasi yake kuchukuliwa Bremer kutoka Juventus.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta anataka kumlinda beki wake hadi hapo mapumziko ya mechi za kimataifa za kirafiki zitakapopita na kurudi uwanjani kwenye Ligi Kuu England kuwakaribisha Man City, Machi 31.

Amecheza mechi 26 kwenye Ligi Kuu England msimu huu, akiunda kombinesheni matata kabisa na William Saliba, kuifanya Arsenal kuwa na ukuta mgumu kabisa, ikiwa imeruhusu mabao 24 tu.

Gabriel mwenye umri wa miaka 26, ameungana na kundi dogo la wachezaji majeruhi kwenye kikosi cha Arsenal, sambamba na Gabriel Martinelli, ambaye pia hakuitwa kwenye kikosi cha Brazil.

Thomas Partey naye hakujiunga na Ghana kwa kuwa bado hajapona vyema na Jurrien Timber anapambana na muda kupona haraka.

Baada ya mechi ya Man City, Arsenal itakipiga na Luton na Brighton kabla ya kurusha kete yake ya kwanza kwenye mchezo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich, Uwanja wa Emirates.

See also  YOUNG AFRICANS YAICHAPA SIMBA KWENYE KARIAKOO DERBY
Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

KESI YA PAULINE GEKUL BADO MBICHI
HABARI KUU Mahakama Kuu Kanda ya Manyara, imepanga kusikiliza rufaa...
Read more
REASONS AS TO WHY MANY FARMERS RESORT...
Requires minimum investment to start with, in comparison to other...
Read more
WAJANE WASIMULIA UGUMU WANAOPITIA KULEA WATOTO BILA...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
NCHI ZENYE KIWANGO KIKUBWA CHA DEMOKRASIA AFRIKA...
Makala. Bara la Afrika bado linakabiliwa na Changamoto kubwa kwenye masuala...
Read more
AJALI YA NGARAMTONI ARUSHA YAUA RAIA WA...
HABARI KUU Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply