SABABU WAZIRI MKUU WA IRELAND LEO VARADKAR KUJIUZULU

0:00

NYOTA WETU

Waziri Mkuu wa Ireland Leo Varadkar ametangaza kujiuzulu.

Varadkar (45) alikiongoza Chama cha Fine Gael tangu mwaka 2017 na kushika nafasi ya Uwaziri Mkuu mara mbili.

Akitoa tangazo hilo kwa hisia kubwa, Bw.Varadkar amesema sababu zake za kujiuzulu ni za binafsi na za kisiasa.

“Baada ya miaka 7 kwenye ofisi, sidhani kama mimi ni mtu bora zaidi kwa kazi hii”

“Naamini Kiongozi mpya atakuwa na nafasi nzuri zaidi yangu, kupata viti kwa ajili ya Chama cha Fine Gael katika uchaguzi mkuu ujao”

“Wanasiasa nao ni binadamu na tuna mapungufu, tunajitahidi lakini inafika hatua hatuwezi tena, hivyo tunaacha na kusonga mbele”.

Varakdar alikuwa mtu mwenye umri mdogo kuliko wote kuwahi kushika nafasi ya Uwaziri Mkuu nchini Ireland akiwa na umri wa miaka 38.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  SABABU JOSEPH SELASINI KUMLIPA JAMES MBATIA MILIONI 80
Don't miss out!
Invalid email address