WAZIRI DOROTHY ATOA MBINU YA KUDHIBITI UNYANYASAJI WA WANAWAKE NA WATOTO

0:00

HABARI KUU

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima ametoa wito kwa viongozi kuhakikisha udhibiti wa wimbi la watoto wanaokimbilia kuishi na kufanya kazi mitaani unaenda sambamba na kuimarisha Kamati za Ulinzi wa Watoto na Wanawake katika mamlaka za Serikali za mitaa.

Dkt. Gwajima ametoa wito huo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara yake Wilaya za Kigamboni na Ilala Mkoani Dar Es Salaam kwa lengo la kufuatilia jinsi gani mkoa unadhibiti wimbi la watoto waishio na kufanya kazi mitaani.

Amebainisha kwamba, kwa mujibu wa Mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kamati hizo zipo katika ngazi za kijiji, mitaa na kata ambapo, viongozi wa Serikali ngazi husika ndiyo wenyeviti na makatibu ni walimu au wataalamu wa kisekta.

Amesema, kundi kubwa la watoto hao lilipaswa kuwa shuleni lakini kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo kulegalega kwa kamati hizo zenye wajumbe wa kisekta, utoro wa watoto hao shuleni hukosa ufuatiliaji hadi ngazi ya kaya hivyo hukimbilia mitaani.

“Naombeni viongozi muhakikishe kamati za ulinzi wa wanawake na watoto zinapata idadi ya watoto waliotoroka shuleni sambamba na kubaini kaya wanazotoka ili kufanya uchambuzi wa mazingira ya kaya hizo na kuchukua hatua za maendeleo na ustawi wa jamii ili watoto hao wanaporejeshwa nyumbani wasitoroke tena,” alisema.

Aidha amesisitiza, Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii wakishirikiana na Wadau wa maendeleo kusaidia kuchambua na kushauri juu ya ufumbuzi wa changamoto za kimaendeleo na kiustawi kwenye kila kaya wanakotokea watoto wanaoonekana kuwa na changamoto ili kudhibiti kabla watoto hao hawajakimbia shuleni na kwenye familia.

See also  WATU ZAIDI YA 100000 WALIVYOKIMBIA VITA DRC
Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

SABABU HIZI HUCHANGIA KUNENEPA HATA BILA KULA...
MAKALA FUPI Tunaposikia maneno kama "kunenepa" au "kunenepa kupita kiasi",sisi...
Read more
AHMED ALLY AIBUKIA KWA FRED MICHAEL KOUBLAN
MICHEZO Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed...
Read more
SUALA LA PACOME NA CAREN SIMBA LIKO...
NYOTA WETU Mrembo Caren Simba amejikuta kwenye wakati mgumu wa...
Read more
FEISAL SALUM "FEI TOTO" APELEKA KILIO YANGA...
MICHEZO Kiungo Feisal Salum Fei Toto amepeleka kilio Jangwani kwa...
Read more
MAHAKAMA YAJIFUNGA KWA KAULI YA JAJI MKUU
HABARI KUU Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Ibrahim...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply