MASHABIKI WA CHELSEA WAANDIKA BARUA KULAUMU UONGOZI

0:00

MICHEZO

Umoja wa Mashabiki wa klabu ya Chelsea wameandika barua kwenda kwa wamiliki wa klabu hiyo, Todd Boehly na Behdad Eghbali wakisema timu hiyo imekuwa kichekesho ndani na nje ya uwanja.

Barua hiyo ililaumu uongozi wa klabu hiyo na kuainisha mambo mbalimbali yanayowagusa mashabiki wa klabu hiyo tangu mwaka 1980.

Todd Boehly na kampuni ya Clearlake Capital waliinunua Chelsea Mei 2022 na wametumia zaidi ya Pauni Bilioni 1 kwenye usajili wa wachezaji.

“Malengo yetu kama wamiliki yako wazi. Tunataka kuwafanya mashabiki wajivunie klabu hii,” alisema Boehly kwenye taarifa yake wakati mpango wa kuinunua klabu hiyo ulipothibitishwa.

Ingawa, barua kutoka kwa Umoja wa Mashabiki wa klabu hiyo inaonesha kwamba bado hawajaridhishwa na namna inavyoendeshwa.

“Umoja wa Mashabiki wa Chelsea unasikitika kuamini kwamba tunakaribia kama sio tayari tunashuhudia kupuuzwa kwa maoni ya mashabiki yanayoweza kubadili matokeo ya timu uwanjani,” ilisema barua hiyo.

“Kama hali haitabadilika, inaweza kusababisha mashabiki kuzomea, hasa kwenye mechi zinazooneshwa kwenye televisheni na baadhi ya mashabiki kujipanga kuandamana kupinga.

Umoja huo pia ulisema kukosekana kwa mawasiliano kwenye mambo mbalimbali unawachanganya mashabiki wa klabu hiyo.

“Hali ya furaha kwa sasa miongoni mwa mashabiki imeshuka sana na haiwezi kupuuzwa.

“Hisia ni kwamba klabu imekuwa kichekesho ndani na nje ya uwanja,” iliongeza barua hiyo.

“Mashabiki wanasema kwamba kwa sasa inaonekana kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na imani na uongozi wa klabu hiyo, hasa kundi linaloenda uwanjani kutokana na kupungua kwa mawasiliano. Mashabiki wengi wanahofu kuhusu hatima ya muda mfupi na mrefu kwenye klabu yetu.”

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

SENEGAL INAUGURATES BASSIROU DIOMAYE FAYE AS YOUNGEST...
PROLIFIC NEWS
See also  Muhimbili watoa orodha ya majeruhi ajali ya Kariakoo
Senegal marked a historic moment on Tuesday as Bassirou...
Read more
BITEKO AZUIA LIKIZO ZA WAFANYAKAZI WA TANESCO
HABARI KUU Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt....
Read more
SABABU YA PRINCE DUBE KUOMBA KUONDOKA AZAM...
MICHEZO Klabu ya Azam FC imethibitisha kupokea barua kutoka kwa...
Read more
TISHIO JIPYA LA DAWA ZA KULEVYA
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
Mkuu wa Wilaya Morogoro Rebeca Nsemwa ameagiza...
DC Rebbeca amesema Diwani huyo amejenga vibanda vya kufanyia biashara...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply