BUNGE LA TANZANIA LAKANUSHA MADAI YA MBOWE KUHUSU MISHAHARA MIPYA YA WABUNGE

0:00

HABARI KUU

Bunge la Tanzania limekanusha madai yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe ambapo alidai kwamba mishahara ya Wabunge imeongezwa mwaka 2023 kutoka shilingi milioni kumi na tatu (sh.13,000,000/=) hadi shilingi milioni kumi na nane (sh.18,000,000/=)

Madai hayo aliyetoa jana ijumaa tarehe 22 Machi, 2024 alipokuwa anahutubia mkutano wa hadhara Mjini Babati Mkoa wa Manyara

Taarifa ya Bunge imeeleza kuwa taarifa hizo ni uzushi na kueleza kuwa hakuna mbunge aliyeongezewa mshahara na nyongeza ya mishahara ni suala linalozingatia bajeti

“Tunapenda kuujulisha umma kwamba madai hayo ni uzushi na upotoshaji kwa kuwa hakuna Mbunge aliyeongezewa mshahara kama alivyodai. Hivyo, tunapenda kuwashauri na kuwasihi wananchi kupuuza madal hayo ambayo lengo lake ni kuleta taharuki pamoja na kuwagombanisha wananchi na wawakilishi wao”

“Nyongeza ya mshahara ni suala linalozingatia bajeti na hakuna utaratibu wa aina yoyote kama huo ambao umefanyika kwa ajili ya kuwaongezea Waheshimiwa Wabunge mishahara” imeeleza taarifa hiyo ya bunge .

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

TABIA 10 AMBAZO KILA MWANAUME ANAZO
LOVE TIPS ❤ 1. Mwanaume ni mtu mwenye sifa kama...
Read more
TIPS FOR MEN ON HOW TO APPROACH...
Have confidence; not pride. Confidence is attractive, women detest pride Women...
Read more
MAMBO MANNE YANAYOHARIBU MAHUSIANO
1. Shutuma kwa mwenza wako,lawama ,kumsingizia makosa ambayo hajatenda na...
Read more
World No. 7 Lee Zii Jia stunned...
In a match between two friends, a well-prepared Zii Jia,...
Read more
Lille midfielder Angel Gomes has been taken...
The London-born former Manchester United player collided with Reims defender...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Mwanamke Amuua Mpenzi wake kwa Kumkata Sehemu Nyeti

Leave a Reply