WANAOTAJWA KUHUSIKA NA SHAMBULIZI LA KIGAIDI NCHINI URUSI

0:00

HABARI KUU

Ukumbi wa Jiji la Crocus huko Krasnogorsk, kitongoji kilicho kaskazini-magharibi mwa Moscow, unajulikana kwa uenyeji wa maelfu ya watu na kupokea wasanii wengi wa Kimataifa.

Video katika mitandao ya kijamii ilionesha watu kadhaa waliokuwa na silaha wakiingia ndani ya ukumbi huo kabla ya kufyatua risasi na kusababisha watu 60 kufariki na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa.

Shambulio hilo ambalo lilitokea kabla ya kuanza kwa tamasha la Picnic, awali kulikuwa na taarifa kupitia mtandao wa instagram kuwa Bendi maarufu ya rock likuwa imeuza ukumbi huo.
 
Hadi tiketi 6,200 zilikuwa zimeuzwa kwa tamasha hilo, kulingana na vyombo vya habari vya Urusi, lakini bado haifahamiki ni watu wangapi walikuwa ndani wakati wa shambulio hilo.

Hata hivyo, inaarifiwa na Vyombo vya habari vya Urusi kwamba washiriki wa bendi hiyo hawakudhurika wakati wa ufyatuaji huo wa risasi.
 
Zaidi ya wiki mbili zilizopita, Machi 7, 2024 ubalozi wa Marekani mjini Moscow ulitoa tahadhari ya usalama baada ya kupokea ripoti kwamba “watu wenye itikadi kali wana mipango ya kulenga mikusanyiko mikubwa mjini Moscow, ikiwemo matamasha.”

Kufuatia tukio hilo, tayari raia wa Marekani wameshauriwa “kuepuka mikusanyiko mikubwa kwa saa 48 zijazo” ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na ukwepaji wa mashambulio hayo.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Raila Explains Reasons for Calling for Dialogue,...
Raila Odinga, the leader of the Azimio la Umoja -...
Read more
Lafey MP Launches Dam and Borehole Projects...
Lafey Member of Parliament (MP) Mohamed Abdikheir has taken a...
Read more
SABABU ZA KIFO CHA KOCHA WA SIMBA...
MICHEZO
See also  CHELSEA YAIFUNGA MANCHESTER KIMIUJIZA
Polisi nchini Rwanda wameanza uchunguzi wa kifo cha ghafla...
Read more
Mfahamu Didi-Stone mmoja wa watoto 7 wa...
NYOTA WETU Didi-Stone Olomidé ambaye amepewa jina kutokana na mjomba...
Read more
EL CLASSICO YA KIBABE LEO KUMBEBA NANI...
MICHEZO Ligi Kuu Uhispania inaendelea tena leo Aprili 21, 2024...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply