BILA NGUMI TANZANIA INGETOKA PATUPU MASHINDANO YA AFRIKA GHANA

0:00

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

MICHEZO



Kikosi cha Timu ya Taifa ya Ngumi ya Tanzania maarufu kama “Faru Weusi wa Ngorongoro” wamefanikiwa kuiheshimisha Tanzania katika michezo ya 13 ya Afrika (All African Games 2023) Jijini Accra nchini Ghana inayofungwa rasmi usiku wa leo katika Jiji hilo.

Kikosi hicho kimefanikiwa kushinda Medali 3 za shaba katika mashindano hayo kutoka kwa wachezaji Light Heavyweight Yusuf Changalawe (Nahodha), Lightweight Ezra Paulo Mwanjwango na Cruiserweight Musa Maregesi.

Wachezaji wote hao wanatokea katika Klabu ya Ngome inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)

Katika sherehe za utoaji wa medali kwa washindi katika mchezo wa ngumi, iliyofanyika usiku wa Machi 23, 2024 katika ukumbi wa Bukom Arena, Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirikisho la Ngumi Bara la Afrika (AFBC) alikuwa kuwa mgeni rasmi katika kuwavalisha washindi wa Uzani wa Ligh Heavyweight 80kg kwa Wanaume na Cruiserweight 86kg, ambapo Changalawe na Maregesi walikuwa moja ya washindi katika uzani hizo.

Kikosi hicho cha Faru Weusi wa Ngorongoro pamoja na wachezaji wa michezo mingine walioiwakilisha Timu Tanzania katika michezo hiyo, wanatarajia kurejea Dar es salaam Machi 25, 2024 saa 9.40 usiku.

Aisha, kikosi hicho kikirejea kitaendelea na mazoezi ya kujiandaa kushiriki mashindano ya Mandela “Mandela Cup” yatakayofanyika Durban, Afrika ya Kusini kuanzia tarehe 15-23 April, 2024.

Related Posts 📫

BUSINESS MODELS
A business model refers to the way a company creates,...
Read more
SIGNS THAT YOU ARE TAKING YOUR PARTNER...
Read more
KAA Confirms Adani as Contractor for Major...
The Kenya Airports Authority (KAA) has confirmed that it has...
Read more
VLADIMIR PUTIN ATOA KAULI NZITO DHIDI YA...
HABARI KUU
See also  Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain wanaanda zaidi ya Pauni 80 milioni kwa ajili ya kutuma ofa kwenda Manchester United ili kuipata saini ya Mshambuliaji wa timu hiyo na England, Marcus Rashford katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.
Rais wa Urusi Vladmir Putin amekiri kwa mara...
Read more
LaMelo Ball, Hornets try to cool off...
The Magic and the Hornets, who meet on Monday night...
Read more

Leave a Reply