HISTORIA YA VITAL KAMERHE LWA KANYIGINYI NKINGI

0

0:00

NYOTA WETU

Siasa ni taaluma kama itafanywa na wataalamu,siasa ni mpango mkakati wa maendeleo ya taifa kwa miaka mingi,wakati mwingine siasa huhitaji unafiki,majungu, fitina na kujikomba kwa viongozi wakubwa ili kulinda mkate wa watoto au kuendelea kujikomba ila kupanda vyeo au kulamba teuzi hii tabia kitaalamu huitwa Sycophancy ambapo kwa kiswahili fasaha ni ubarakala.

Wanasiasa wengi marafiki barani Afrika huwa wanakubaliana vizuri lakini baadae wanasalitiana na hatimae kuuana kutokana na tamaa ya mali, madaraka na nguvu za kijeshi na intelijensia. Mfano wa marafiki waliosalitiana ni Muammar Mohammed Abu Minyar Gaddafi na Khalifa Belqasim Haftari Libya, Thomas Sankara na Blaise Compaore, Milton Obote na Yoweri Kaguta Museveni.

Nchini Congo Kuna kadhia nzito inayomuandama spika wa zamani wa Bunge la Congo ndugu Vital Kamerhe baada ya kusalitiwa na Raisi wa sasa wa Congo ndugu Felix Tshisekedi.

Je ndugu Vital Kamerhe ni nani?.

Ndugu Vital Kamerhe alizaliwa tarehe 4/3/1959 nchini Congo enzi za utawala wa Wabeligiji,ni Mzalendo kindakindaki na mwanasiasa mkongwe nchini Congo,ni miongoni mwa watu wa siri kwenye utawala wa Raisi wa sasa wa Congo ndugu Felix Tshisekedi na ni kiongozi mkuu wa chama Cha (UNC) yaani Congolese National Opposition party.

Hapo awali alikuwa spika wa Bunge tukufu la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuanzia mwaka 2006 mpaka mwaka 2009 ambapo alijiuzulu nafasi yake kutokana na kashfa za rushwa na upendeleo huku wengine wakidai kwamba alikuwa kibaraka wa Generali Yoweri Kaguta Museveni na Paul Kagame . Lakini sababu kubwa ya kujiuzulu kwake ni kumpinga waziwazi Raisi Joseph Kabila kutokana na uvamizi wa majeshi ya Uganda na Rwanda eneo la kivu.

Baada ya kustaafu uspika alianzisha chama Cha upinzani Cha UNC mwaka 2011 kwa lengo la kuwa Raisi wa Congo.

Uchaguzi mkuu wa Congo wa mwaka 2011 ndugu Vital Kamerhe alikuwa miongoni mwa wagombea wa uraisi ingawa alianguka patupu mbele ya Joseph Kabila, ambapo ndugu Vital Kamerhe alipata kura asilimia 7.74%

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2018 chama cha UNC cha Vital Kamerhe kiliamua kumuunga mkono Felix Tshisekedi kwa makubaliano yafuatayo mosi ndugu Vital Kamerhe kuwa waziri mkuu, UNC kupewa viti 15 bungeni na ulinzi na usalama kwa wanachama wake.Vital Kamerhe ana ushawishi mkubwa eneo la Kivu ambapo kuna wakimbizi wengi wenye asili ya Rwanda yaani Banyamurenge na wengine wenye asili ya uganda . Alizunguka nchi nzima kumnadi Felix Tshisekedi na hatimae Tshisekedi akawa Raisi ingawa kuna madai kwamba Martin Madidi Fayuru alishinda uchaguzi lakini Joseph Kabila aliamua kumpa nchi Felix Tshisekedi ili amlinde kisiasa na hofu ya kushtakiwa baada ya kumaliza uongozi wake. Joseph Kabila aliamua kumtosa mgombea wa chama chake ndugu Emmanuel Ramazani Shadai ambaye walikuwa marafiki tangu maisha ya utoto na Jeshi la Wananchi Tanzania.

See also  LHRC KUMSHITAKI OSCAR OSCAR

Baada ya uchaguzi ndugu Vital Kamerhe akaona kwamba amesalitiwa na Felix Tshisekedi hivyo akaamua kuanza harakati za chinichini kudai haki za chama chake cha UNC na hapo ndipo ugomvi mkubwa kati yake na Raisi Felix Tshisekedi ukazuka.

Mwezi April mwaka 2020 ndugu Vital Kamerhe alikutwa na hatia ya uhujumu uchumi, ufisadi na utakatishaji fedha wa Zaidi ya dola milioni 48 za Marekani.Mahakama ya juu ya Kinshasa ikamhukumu miaka 20 jela kwa ushahidi wa mwendesha mashtaka wa serikali ingawa sipo kwa minajiri ya kumtetea ndugu Vital Kamerhe.

Maisha ya utoto ya Vital Kamerheā€¦ā€¦ā€¦.

Vital Kamerhe alizaliwa wilaya ya Bukavu tarehe 4/3/1959 jina lake kamili ni Vital Kamerhe Lwa Kanyiginyi Nkingi ,ni mtoto wa kiume wa Constantin Kamerhe Kanyiginyi na mama yake anaitwa Alphonsine Mwa Nkingi.Anatoka katika kabila dogo la Shi kwenye jamii ya Walungu. Ana mke na watoto tisa.

Alianza elimu ya msingi huko Bukavu na baadae akafanikiwa kwenda mjini Goma,huko nako akahama na kwenda kusoma Jimbo la Kasai ambapo alihitimu elimu ya msingi mwaka 1975.

Mwaka 1976 alijiunga na chuo cha Sadisana na baadae chuo cha Mbuji _Mayi na kufikia mwaka 1980 alikuwa na Shahada ya uongozi na siasa,alimudu lugha zaidi ya tano ambazo ni Kifaransa,lingala, kiswahili na Tshiluba.

Mwaka 1987 alisoma chuo kikuu cha Kinshasa shahada ya uchumi na kwakuwa alikuwa na Shahada ya uongozi na siasa ikabidi abaki chuoni kama mwalimu.

Akiwa mwalimu wa chuo kikuu cha Kinshasa alianza harakati za kuwa mwanasiasa na alijiunga na Chama cha UDPS chama hicho kilikuwa na wanasheria, wanazuoni na majasusi kadhaa akiwemo Vincent de Paul Lunda Bululu na Moize Lerwaa.

Kuanzia mwaka 1993_1995 ndugu Vital Kamerhe alikuwa kwenye nyazifa mbalimbali za kisiasa nchini Congo.

Mfano mwaka 1993 Raisi wa Congo Generali Mobutu Sese Seku Kuku Ngendu wa Zabanga (1930_1997) alimteua kama Mkurugenzi wa wizara ya mazingira na utalii kutokana na umahiri wake wa lugha.

Mwaka 1994 akateuliwa kuwa mpanga mipango wa ofisi ya waziri mkuu wa Congo.

Mwaka 1994_1995 akateuliwa kuwa Mkurugenzi wizara ya elimu na tume ya chuo vikuu Congo.

Kuna habari za kijasusi na intelijensia kuwa ndugu Vital Kamerhe alikuwa mojawapo ya wauaji wa siri wa Dikteta Mobutu kwenye kikundi cha Frojemo ambacho kikundi hicho kiliongozwa na Generali Etienne Nzimbi Ngbale Kongo Wa Basa.( Huyu alikuwa binamu wa Mobutu Sese Seku Kuku Ngendu wa Zabanga na aliua watu wengi waliompinga Mobutu.)

Baada ya kuanguka kwa utawala wa Dikteta Mobutu Sese Seku Kuku Ngendu wa Zabanga mwaka 1997 kufuatia operesheni Kitona iliyoanzishwa na Kagame, Museveni, serikali ya Tanzania na Marehemu Profesa Wamba dia Wamba na hatimae Mobutu Sese Seku Kuku Ngendu wa Zabanga akatawafu mwaka 1997 mjini Rabat Morocco.

Laurent Kabila alichukua Nchi ya Congo na kuongoza mpaka mwaka 2001 ambapo aliuawa na walinzi wake Ingawa kuna changamoto, utata na sintofahamu nyingi kuhusu kifo na kadhia ya Laurent Kabila.

Wakati wa utawala wa Laurent Kabila ndugu Vital Kamerhe nyota yake iling’aa kwa sababu aliendelea kupata teuzi mbalimbali mfano alikuwa mshauri wa mambo ya kijeshi na intelijensia wakati huo akifanya kazi chini ya jasusi Etienne_ Richard Mbaya.

Mwaka 1998 aliteuliwa kuwa mkuu wa usalama wa taifa Congo huku akiwa mshauri wa mambo ya fedha chini ya Raisi Laurent Kabila.

Baadae akawa mshauri wa mambo ya kijeshi namba mbili nchini Congo baada ya Generali Denis Kalume.

Ndugu Vital Kamerhe ameshiriki kwenye midahalo na kongamano kadhaa za kuleta amani na upatanishi nchini Congo mfano mvutano wa kisiasa Congo mwaka 2002 baada ya kifo Cha Laurent Kabila.

Viongozi kadhaa wa maziwa makuu walikutana kujadili hatma ya mzozo wa Goma au Kivu.Raisi wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, Rwanda Paul Kagame, Angola Jose Edwardo Dos Santos, Msumbiji Joachim Chissano ,Burundi Pierre Buyoya na Benjamin Mkapa.

Mwaka 2003 Vital Kamerhe aliteuliwa kuwa waziri wa habari na mawasiliano ya kimataifa.

Mwaka 2004 alikuwa mstari wa mbele kwenye kampeni za uraisi nchini Congo ambapo Joseph Kabila alishinda kwa asilimia 70 kupitia chama Cha PPRD.

See also  WAYS ON HOW TO FIGHT FOR YOUR MARRIAGE

Katika uchaguzi huo ndugu Vital Kamerhe alichaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Bukavu na decemba mwaka 2006 ndugu Vital Kamerhe alichaguliwa kuwa spika wa Bunge tukufu la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mwaka 2009 ndugu Vital Kamerhe akiwa kama spika wa Bunge la Congo alimuita Raisi Joseph Kabila bungeni kumuhoji bungeni kuhusu kadhia ya Joseph Kabila kuruhusu Operesheni Umoja Wetu ambapo Jeshi Ia Rwanda liliingia Congo na kufanya ujasusi na uasi huku bunge likiwa halijui.

Tarehe 21/1/2009 ndugu Vital Kamerhe alifanya mahojiano na Redio Okapi huku akionyesha masikitiko makubwa kwa Raisi Joseph Kabila kuwa muoga kwa Kagame na Museveni ambao wana makundi ya waasi Congo.

Mzozo wa kivu una zaidi ya miaka 60 bado hali ni tete huku ndugu Vital Kamerhe akiamini kwamba Congo haina viongozi wazalendo ambao wanaweza kumkemea Kagame na Museveni.

Vital Kamerhe alisema kwamba Raisi Joseph Kabila amekosa sifa za kuwa Raisi wa Congo kwa sababu amekiuka katiba ya nchi hiyo kifungu namba 213 ibara ya 8 ambacho kinasema kwamba operesheni za kijeshi lazima zibarikiwe na bunge tukufu.

Tarehe 25/3/2009 aliamua kujiuzulu kazi ya uspika wa bunge la Congo kutokana na kutokuwa na imani na Raisi Joseph Kabila huku wengine wakidai kwamba ni kashfa za rushwa na ufisadi.

Tarehe 14/10/2010 ndugu Vital Kamerhe alijiondoa chama Cha PPRD cha Joseph Kabila na kuanzisha chama chake cha UNC.

Katika uchaguzi wa mwaka 2011 aligombea na kupata asilimia 7.74%.

Katika uchaguzi wa mwaka 2018 ndugu Vital Kamerhe aliamua kumuunga mkono Felix Tshisekedi na akawa mpiga kampeni Nchi nzima.

Huyo ndio Vital Kamerhe Lwa Kanyiginyi Nkingi ambaye yuko jela kutokana na kesi ya uhujumu uchumi, ufisadi na utakatishaji fedha wa Zaidi ya dola milioni 48 za Marekani.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading