JOAN LAPORTA NA BARCELONA YAKE WAKATAA KUMUUZA LAMINE YAMAL

0

0:00

MICHEZO

Rais wa FC Barcelona Joan Laporta amekiri kuwa klabu hiyo imekataa ofa ya Pauni milioni 200 (sawa na Sh bilioni 551) kwa ajili ya Lamine Yamal.

Taarifa hiyo imetolewa hivi karibuni, kupitia kwa wakala Jorge Mendes baada ya kutoa mapendekezo kuhusu mshambuliaji huyo wa Blaugrana.

FC Barcelona imekataa kabisa ofa kutoka klabu ya Ufaransa ya PSG kwa sababu wanafikiria mchezaji huyo atawafaa katika siku za usoni.

Hivi ndivyo jinsi Laporta alivyosema: “Tumepokea ofa kwa ajili ya baadhi ya wachezaji wetu, kama Lamine Yamal, kwa ada ya euro milioni 200, na alisema hapana. Kwa sababu tunamuamini kijana, kwa sababu ni nguzo ya timu hapo baadae.

“Kwa sababu tuna imani na kijana, ana kipaji, na bado tunamuhitaji,” alisema Laporta, ambaye alisema klabu hiyo inapitia kipindi kigumu kwa sasa.

Hali ya kifedha ya Barcelona sio nzuri sana, hivyo inashawishi kutaka kumuuza mchezaji huyo kwani kutasaidia kuipatia kipato cha fedha klabu hiyo kutoka kwa mhezaji wao mmoja na hiyo ni njia pekee ya kusaidia kuweka sawa matumizi ya fedha.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Droo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imekamilika huku vigogo 8 waliofuzu hatua hiyo wakibaini wapinzani wao.Kama kawaida, Washika Mitutu, Arsenal wamepangwa dhidi ya Bayern Munich kwenye hatua hiyo huku Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo, Manchester City wakikutanishwa na Mabingwa wa kihistoria, Real Madrid.Barcelona imepewa PSG huku Atletico Madrid ikipewa Borussia Dortmund.DROO KAMILI Arsenal šŸ“󠁧󠁢󠁄󠁮󠁧ó æ vs. šŸ‡©šŸ‡Ŗ Bayern MunichAtletico Madrid šŸ‡ŖšŸ‡ø vs. šŸ‡©šŸ‡Ŗ DortmundReal Madrid šŸ‡ŖšŸ‡ø vs. šŸ“󠁧󠁢󠁄󠁮󠁧ó æ Manchester CityParis Saint-Germain šŸ‡«šŸ‡· vs. šŸ‡ŖšŸ‡ø BarcelonaMshindi kati ya Arsenal na Bayern Munich atachuana na mshindi kati ya Real Madrid na Manchester City kwenye hatua ya nusu fainali.Mshindi kati ya PSG na Barcelona atachuana na mshindi kati ya Atletico Madrid dhidi ya Borussia Dortmund.
Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading