MACKY SALL AMPONGEZA BASSIROU DIOMAYE FAYE KUSHINDA URAIS

0

0:00

HABARI KUU

Rais wa Senegal anayemaliza muda wake, Macky Sall amempongeza mgombea wa upinzani, Bassirou Diomaye Faye kwa ushindi alioupata huku mshindani wake wa karibu, Amadou Ba akikubali kushindwa katika uchaguzi huo.



Baada ya mgombea huyo wa chama tawala, Amadou Ba kutambua ushindi wa Faye katika duru ya kwanza na kutoa pongezi zake, Sall, ambaye alishinda chaguzi za mwaka 2012 na 2019, amesema ā€œnapongeza maandalizi mazuri ya uchaguzi na nampongeza mshindi, Bassirou Diomaye Faye ambaye mwenendo wa kura unaonyesha kwamba ameshinda.ā€

Mgombea huyo wa upinzani aliyeshinda hajawahi kushika nafasi ya kuchaguliwa ya kitaifa na bado hajazungumza hadharani tangu uchaguzi wa Jumapili Machi 24, 2024, uliofuatia miaka mitatu ya machafuko na mgogoro wa kisiasa.

Mpinzani wake mkuu kutoka muungano wa chama tawala, Amadou Ba ametambua ushindi wa Faye katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo na akatoa pongezi zake, ilisema taarifa.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Kwanini Mchezaji Roberto Firmino Amegeukia Kazi ya Injili?
Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading