UMMY MWALIMU ATAJA MAFANIKIO YA WIZARA YA AFYA KWENYE UTAWALA WA RAIS SAMIA

0

0:00

HABARI KUU

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema sekta ya afya imekua kwa kiwango kikubwa kwenye miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan kiasi cha kuvutia watu kutoka nchi jirani kuja kutibiwa Tanzania ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Waziri Ummy amesema Sekta ya Afya kwa sasa imejikita zaidi kwenye tiba za kisasa na kwamba kwa upande wa vipimo ambapo mashine za CT-Scan zimeongezwa kutoka 13, kisha 32 na sasa ziko 45 kwa nchi nzima.

Kwa upande wa Ultra sound amesema kwa sasa zinapatikana mpaka kwenye zahanati ambapo kabla ya Rais Samia kuingia madarakani kulikua na mashine za ultra sound 476 ila sasa zipo 665 na kwamba zinasaidia sana matibabu hasa kwa mama wajawazito.

Upande wa mashine za moyo amesema tumetoka kwenye mashine moja mpaka nne, kiasi cha kuvutia nchi nyingi kuja kupata huduma za afya nchini ikiwemo Malawi, Uganda, Kenya, Comoro, Burundi na nyingine nyingi.

Waziri Ummy amesema hayo jijini DSM mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye kilele cha Wiki ya Kurasa 365 za Mama Vol. 3 iliyoandaliwa na Clouds Media Group. Ametumia wasaa huo kuwataka Watanzania kufanya mazoezi na kupunguza matumizi ya vyakula vya mafuta, sukari, chumvi na wanga ili kutunza afya zao.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  JACOB ZUMA ANUSURIKA KUFA
Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading