MALAM BACAI SANHA JR AHUKUMIWA MIAKA 6 JELA KWA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA

0

0:00

HABARI KUU

Mahakama nchini Marekani imemuhukumu kifungo cha zaidi ya miaka sita mtoto wa Rais wa zamani wa Guinea-Bissau Malam Bacai Sanha Jr almaarufu kama ā€Bacaizinhoā€ kwa makosa ya usafirishaji wa Kimataifa wa dawa za kulevya.

Sanha Jr (52), ni mtoto wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Malam Bacai Sanha, aliyeongoza kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2012 alipofariki.

Sanha Jr anahusishwa na Mapinduzi yaliyofeli Februari 2022. Alikabidhiwa kwa Serikali ya Marekani Agosti 2022 baada ya kukamatwa nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa FBI,

ā€Sanha Jr alikuwa akisafirisha dawa kwa nia ya kupata pesa za kufadhili mapinduzi yatakayomuwezesha kuwa Rais wa Guinea-Bissau ambapo walipanga kuanzisha utawala wa dawa za kulevyaā€.

Amewahi kushikilia nafasi mbalimbali katika Serikali ikiwemo ya mshauri wa masuala ya Uchumi wa baba yake wakati alipokuwa Rais.

Guinea-Bissau ni kitovu maarufu cha biashara haramu ya dawa za kulevya. Ni njia kuu inayotumika kusafirisha dawa hizo kutokea Amerika Kusini kwenda Ulaya.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Brentford have signed defender Sepp van den Berg from Liverpool in a deal worth up to Ā£25m.
Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading