SABABU ZIWA TANGANYIKA KUFUNGWA MIEZI MITATU

0:00

HABARI KUU

Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanza kutekeleza mpango wa kulipumzisha Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma kuanzia Mei 15 hadi Agosti 15, 2024 ambapo shughuli za uvuvi zitazuiwa katika kipindi hicho.

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Salum Kalli, amewaambia wadau, viongozi na wavuvi wanaotumia ziwa hilo kuwa zoezi hilo ni sehemu ya kukuza sekta ya uvuvi nchini, kwa kuwa hatua hiyo itasaidia ongezeko la samaki na soko katika siku za usoni kutokana na uwepo wa samaki wa kutosha.

Kalli, amesisitiza juu ya umuhimu wa zoezi hilo katika Ziwa Tanganyika akisema ni kitovu cha mazao ya samaki kutokana na mazalia kuwa mengi na yenye kukidhi mahitaji ya watumiaji.

Ofisa Uvuvi Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ambakisye Simtoe amewataka wadau wa uvuvi kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha juu ya kupumzishwa kwa Ziwa Tanganyika ili kuchochea ongezeko la samaki katika ziwa hilo.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Kwanini Mali Imesitisha Safari za Ndege?
Mashirika ya ndege ya Mali yamesitisha safari za ndani...
Read more
CLATOUS CHAMA Agomea Ngao ya Jamii
CLATOUS CHOTA CHAMA ASUSIA NGAO YA JAMII.. Clatous Chama, kugomea kushangilia...
Read more
MADAM RITA KWENYE MAOMBI YA NDOA
NYOTA WETU Jaji wa shindano la BSS , Rita Poulsen baada...
Read more
Canada have failed in an appeal to...
Russia were dropped from gold to bronze in the competition...
Read more
18 COSTLY MISTAKES THAT WIVES MAKE
PROLONGING SILENT TREATMENT WHEN OFFENDED TO SHOW YOU ARE ANGRYThis...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply