SABABU SINGAPORE KUKATAA KUANDAA MICHEZO YA JUMUIYA YA MADOLA

0:00

MICHEZO

Singapore imekataa kuandaa Michezo ya Jumuiya ya Madola ya mwaka 2026, huku utaratibu wa kutafuta mwenyeji mwingine ukiendelea, imefahamika.

Jimbo la Victoria la Australia lilijondoa kuwa mwenyeji wa awali wa michezo hiyo Julai mwaka jana kwa madai ya kuongezeka kwa gharama za uendeshaji.

Malaysia nayo iliyopewa nafasi ya kuwa mwenyeji na kupewa Pauni milioni 100 (sawa na Sh bilioni 326) kusaidia gharama za maandalizi, mwezi uliopita walikataa ofa hiyo.

Katika taarifa yake ya michezo, Jumuiya ya Madola ilieleza kuwa Singapore iliamua kutowasilisha ombi lolote. Singapore haijawahi kuandaa michezo hiyo.

Imebaki miaka miwili tu kabla ya kufanyika kwa michezo hiyo na hakuna nchi iliyokubali kuwa mwenyeji.

Msemaji wa Shirikisho la Michezo la Jumuiya ya Madola alisema hivi karibuni kuwa ilikuwa na mazungumzo ya kina na wanaotarajia kuandaa michuano hiyo, na kuahidi kutoa msaada wa Pauni milioni 100 ili kuisaidia nchi itakayokubali baada ya Victoria kujitoa.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Actress Kemi Lala Akindoju expresses her views...
Actress Kemi Lala Akindoju has ignited a thought-provoking dialogue surrounding...
Read more
Pep Guardiola has shocked viewers of the...
His Manchester City side had just played out a frustrating...
Read more
AISHI MANULA KUIKOSA AL AHLY
MICHEZO Klabu ya Simba imepata pigo baada ya mlinda mlango...
Read more
No timeline for Le Normand's return from...
Atletico Madrid cannot provide a timeline for defender Robin Le...
Read more
King becomes first female athlete to be...
NEW YORK, - Billie Jean King has been awarded the...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Newcastle beat Arsenal 1-0 to deliver Gunners a blow in title race

Leave a Reply