YANGA YAWASILISHA MALALAMIKO HAYA CAF

0:00

MICHEZO

Klabu ya Yanga imewasilisha malalamiko kwenda CAF kuhusu uwezekano wa makosa ya kiutawala na upangaji matokeo wakati wa mechi ya robo fainali dhidi ya Mamelodi Sundowns iliyochezwa tarehe 05 Aprili 2024 kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld mjini Pretoria, Afrika Kusini.

Barua ya Mkurugenzi wa Sheria wa klabu hiyo, Adv. Simon Patrick kwenda CAF imebainisha kuwa malalamiko hayo yanahusu kukataliwa kwa goli la wazi la Yanga Sc lililofungwa mnamo dakika ya 57 na Aziz Ki Stephane na timu nzima ya waamuzi wakiongozwa na Mbwana Dahane Beida kutoka Mauritania.

“Licha ya kuwepo kwa teknolojia ya Video Assistant Referee (VAR), Bw. Beida na timu yake, akiwemo Bw. Daniel Ayi (Video Assistant Referee kutoka Ghana) na Bw. Jerson Dos Santos (Msaidizi wa VAR kutoka Angola), kwa makusudi walizembea kukagua tukio la goli kupitia VAR, na hivyo kupuuza kanuni za uchezaji haki na usawa katika soka.” imesema barua hiyo.

“Tunadai kuwa hatua hizo za timu ya waamuzi zinaonyesha jaribio la kimakusudi la kushawishi matokeo ya mechi kwa upande wa Mamelodi Sundowns, ikiwa ni kesi mbaya ya upangaji matokeo.”

“Hili limeonekana wazi pale ambapo uchaguzi wa maamuzi ya kutumia VAR ulijikita zaidi katika faulo zilizofanywa na Young Africans Sports Club kutafuta uwezekano wa kadi nyekundu huku wakipuuza fursa halali ya kufunga mabao.”

“Inatia wasiwasi kuwa licha ya uwekezaji mkubwa katika teknolojia ya VAR, jukumu lake katika kuhakikisha usawa na usahihi katika maamuzi muhimu ya mechi halikuzingatiwa. Tukio hili linazua maswali kuhusu uadilifu wa viwango vya waamuzi na ufanisi wa VAR katika kuzingatia kanuni za uchezaji wa haki katika mashindano ya soka.”

See also  TP MAZEMBE YAKANUSHA TAARIFA ZA KIFO CHA RAINFORD KALABA

“Tunaomba uchunguzi wa kina kuhusu suala hili kufanywa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ili kubaini ushahidi wowote wa makosa ya kiutawala au upangaji matokeo. Vitendo kama hivyo vinaharibu ari ya mchezo na lazima vishughulikiwe mara moja ili kudumisha uaminifu wa mashindano ya kandanda chini ya CAF.”

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

CAS YAISHIKILIA USM ALGER KILA SEHEMU
MICHEZO Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) imetupilia mbali ombi...
Read more
TOFAUTI KATI YA FANGASI NA PID NI...
AFYA Fangasi ukeni na PID (Pelvic Inflammatory Disease) ni magonjwa...
Read more
Victor Olatunji scores on his first Champions...
Sparta Prague made a strong return to the Champions League...
Read more
Cheng Su Yin and Hoo Pang to...
Shuttler Cheng Su Yin’s hunger and willingness to learn could...
Read more
Makocha wanaohusishwa kumrithi Mauricio Pochettino Chelsea
MICHEZO Majina ya Makocha Thomas Frank wa Brentford na Vincent...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply