MAPENZI
NAKUKUMBUSHA TU SI KWA UBAYA
Usikubali kuoana na mbadala maana hitaji la moyo wako bado lipo palepale.
- Isiwe kwasababu amekuacha fulani basi ukaamua uoane na fulani kuziba nafasi iliyoachwa wazi imekula kwako
Utakutana na majaribu mengi katika mahusiano hayo kwasababu ulioana na mbadala tarajia kukutana na watu wa ndoto zako wakiwa single na wenye sifa ulizozihitaji tangu awali.
Kama hitaji lako lilikuwa ni pilau usile wali mweupe kisa umekosa viungo au pilau litachukua muda kuliandaa. Litakuchelewesha kula ukaamua andae wali mbadala wa pilau.
Ndugu yangu hitaji la pilau haliondoshwi kwa kula wali mweupe, hitaji la pilau liko palepale. Usioane na mbadala ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi au kwasababu umechoka kusubiri
- Usiolewe au kuoa mtu kisa umezaa naye eti mlee mtoto pamoja. Mtoto hawezi kuleta upendo kwenu hakika mmoja atakuwa kama house girl ambaye anazaa na kulala na boss wake. Msioane kwa kigezo cha mtoto mbali uwe upendo.
- Usioe au kuolewa na mtu kwa kigezo cha kupata unafuu wa maisha eti ana kazi, pesa au biashara. Akili kijiko hiyo ina matokeo mabaya kuona na mtu ili akusaidie maisha hata kama humpendi.
Kama huamini waulize walioa au kuolewa kwasababu fulani ama upweke, wapate kuhudumiwa au mtoto au walitumia hasira za kuachwa wakaamua kuoana na mtu yeyote tu ili wazibe nafasi iliyoachwa wazi nk
Watakuambia wanapitia nini kwenye ndoa hizo hakika utawahurumia.