SABABU ZA KLABU YA YOUNG AFRICANS KUFUNGIWA KUSAJILI NA FIFA

0:00

MICHEZO

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa taarifa kuwa Klabu ya Young Africans (Yanga) inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC imefungiwa kufanya usajili kwa kukiuka kanuni za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Taarifa imeeleza kuwa uamuzi huo umefanywa na FIFA baada ya klabu hiyo kukiuka Annexe 3 ya Kanuni ya Uhamisho wa Wachezaji (RSTP) ya Shirikisho hilo.

Aidha Yanga haikuingiza uthibitisho wa malipo ya uhamisho wa mchezaji husika (jina halijatajwa) katika Mfumo wa Usajili (TMS), licha ya kukumbushwa kufanya hivyo.

Yanga imetakiwa kutekeleza matakwa hayo ya kikanuni, na kuwasilisha taarifa kwa Sekretarieti ya
Kamati ya Nidhamu ya FIFA ambapo suala hilo limefikishwa kwa ajili ya hatua zaidi.

Kutokana na uamuzi huo wa FIFA, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeifungia klabu hiyo kufanya usajili kwa wachezaji wa ndani.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MFAHAMU JUDITH TULUKA SUMINWA WAZIRI MKUU MPYA...
HABARI KUU Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC),...
Read more
10 RULES OF SEX DURING DATING.
Don't sleep with a woman on the first day of...
Read more
NIKE NA DFB SASA MAMBO NI SAFI...
MICHEZO Uamuzi wa shirikisho la soka Ujerumani kuachana na Kampuni...
Read more
ULEVI KWA VIJANA KILIMANJARO WAWATISHA VIONGOZI
HABARI KUU Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa mwisho wa mwaka...
Read more
TIPS FOR A PERFECT TIMING AND SEX
LOVE TIPS ❤ 11 TIPS FOR A PERFECT TIMING AND...
Read more
See also  Kenyan Government Rolls Out New Digital ID Cards, Sparking Concerns

Leave a Reply