MICHEZO
Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans leo Jumanne (Aprili 16) imeingia mkataba wa mwaka mmoja na kampuni ya Silver General Investment unatoa fursa kwa mashabiki na Wanachama wa timu hiyo kukopeshwa simu na kulipa kwa awamu tofauti.
“Mwanachama na Shabiki wa Young Africans ambaye anahitaji kukopeshwa simu anapaswa kutoa kiasi cha Tsh 75,000 na kiasi kinachobaki analipa kidogo kidogo”
“Ndani ya simu utapata App ya Young Africans ambayo imelipiwa kwa miezi miwili na nusu. Natoa wito kwa Wanachama wa Young Africans SC kuikimbilia fursa hii ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Klabu yako”
“Wataalamu wetu wa Silver General Investment watatoa semina ya namna gani simu hizi za mkopo zinapatikana na zinapaswa kulipiwa. Kimsingi simu hizi hazitalipiwa kwa kutoa hela keshi.
“Watakuwa na mfumo maalum wa kulipia ili kuepukana na matapeli ambao wanaweza kuathiri biashara hii. Tutatumia matawi yetu kuratibisha mfumo mzima wa ukopeshwaji na ulipaji ili kudhibiti mwenendo mzima wa biashara hii” amesema rais wa Young Africans Eng. Hersi Said