AFYA
Kukoma kwa hedhi (Menopause) ni kitendo cha kawaida ambacho hutokea kwa wanawake hasa wanapofikia umri Wa kuanzia miaka 40 na kuendelea ingawa pia walioko Chini ya miaka 40 inaweza ikatokea pia na hii inategemea na pia huendelea baada ya miaka 40.
Kukoma kwa hedhi hutokea pale ambapo mwanamke anakosa kuziona siku zake kwa muda Wa miezi 12 inayofuatana au mwaka mmoja na pia anakuwa hana uwezo Wa kupata ujauzito kama ilivyo kawaida.
Kukoma hedhi hutokea pale ovari zinapokuwa na umri mkubwa na kuzalisha kwa kiwango kidogo homoni ambazo haziwezi kufanya kazi zake kama mwili unavyotaka au unavyohitaji.
Mwili huanza kupata mabadiliko mbalimbali yatokanayo na uzalishaji mdogo Wa Estrogen, Progesterone,Testosterone,Follicle Stimulating Hormone na Luteinizing Hormone.
Mojawapo ya dalili inayoonekana mapema ni kupotea kwa Ovarian Follicles ambazo husaidia kuzalisha mayai ya mwanamke kwenye ukuta Wa ovari hivyo kuruhusu mzunguko Wa damu au kutungika kwa mimba kutokea.
Kuna baadhi ya wanawake hupata ukomo Wa hedhi kutokana na vidonda au upasuaji unaoondoa ovari na sehemu zote zinazohusika.
Kwa baadhi ya wanawake huanza kupata hali hii au tatizo hili miaka minne kabla ya umri Wa kikomo kufika na dalili huendelea hata zaidi ya miaka minne ukishafika ule umri Wa kikomo.
Baadhi ya wengine hupata changamoto hii au dalili za hili tatizo kwa zaidi ya miaka 10 kabla haujafika muda wenyewe na Mara nyingi ni 1 kati ya 10 huangukia hapa wengine huendelea hadi miaka 12 baada ya kupata hedhi ya mwisho.
Kuna mambo mengi ambayo yanaweza kukusaidia kuweza kujua lini utaanza kikomo cha hedhi ikiwa ni pamoja na sababu za kijenetiki na afya ya ovari kwa ujumla.
Perimenopause huanza au hutokea kabla ya Menopause na hiki ni kipindi ambacho homoni huanza kubadilika kujiandaa kwa ajili ya Menopause.
Inaweza kuanza muda wowote kwa miezi michache mpaka miaka kadhaa.Wengi Wa wanawake huanza Perimenopause baada au wakati Wa miaka yao ya 40 ingawa wengine wanaweza wasipitie hatua hii na kwenda moja kwa moja kwenye Menopause.
Zaidi ya 1% ya wanawake huanza Menopause kabla ya miaka 40 na zaidi ya 5% huanza Menopause kati ya miaka 40 na 45 na hii kitaalamu huitwa au hujulikana kama Early/Premature Menopause au Primary Ovarian Insufficiency.
Wakati Wa Perimenopause hedhi hutokea lakini inakuwa sio ya kawaida,inaweza ikachelewa,inaweza ikaruka kipindi kimoja nk.
Pia damu inaweza kuwa nzito au nyepesi.
Hivyo lazima ujue,
Menopause ni kukosa au kukwama kwa mzunguko Wa hedhi kwa zaidi ya mwaka mmoja au miezi 12.
Post menopause ni miaka au kipindi kinachoendelea baada ya Menopause kuanza.
Kila Menopause kwa mwanamke hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke.Dalili huwa mbaya zaidi pale inapotokea ghafla au ndani ya kipindi cha muda mfupi.
Kuna hali ambazo pia huweza kuathiri afya ya ovari kama kansa au dizaini ya maisha Fulani kama V uvutaji Wa sigara husababisha kuongezeka kwa muda kwa dalili za Menopause kuendelea kuonekana.
Zaidi ya dalili na mabadiliko ya Menopause,dalili za Perimenopause na Postmenopause zote zinafanana.
DALILI ZA PERIMENOPAUSE,MENOPAUSE NA POSTMENOPAUS
Baadhi ya dalili za Perimenopause ni pamoja na:-
👉🏿Kutokwa na Jasho usiku mwili mzima.
Na inakadiriwa zaidi ya 75% hupata dalili hizo za Perimenopause wakifikia Menopause.
Dalili za Menopause zilizozoeleka ni pamoja na :-
👉🏿Joto la ghafla mwilini kwa sekunde 30 mpaka Dakika 10 na hali hii huendelea mpaka mwaka mmoja hadi miwili.
👉🏿Kutokwa na jasho jingi mwilini hasa wakati Wa usiku.
👉🏿Ngozi kubadilika rangi na kuwa nyekundu.
👉🏿Kuwa mkavu ukeni.
👉🏿Kukosa usingizi au Insomnia.
👉🏿Usingizi Wa mang’amung’amu.
👉🏿Kuwa na Mood au muonekano usiokuwa Wa kawaida.
👉🏿Maumivu kipindi au wakati Wa tendo la ndoa.
👉🏿Kutokwa na damu isiyokuwa ya kawaida (nzito,nyepesi au yenye alama au mabonge)
👉🏿Kukosa nguvu na kulegea.
👉🏿Viungo kuuma.
👉🏿Maumivu ya mgongo.
👉🏿Maziwa kuwa makubwa au kuongezeka saizi.
👉🏿Maumivu ya maziwa (Matiti).
👉🏿Moyo kwenda mbio.
👉🏿Maumivu ya kichwa.
👉🏿Kuwa na ngozi kavu.
👉🏿Kuwasha kwa ngozi.
👉🏿Kuongezeka uzito na kunenepeana.
👉🏿Kukojoa Mara kwa Mara.
👉🏿Kushindwa kuuzuia mkojo hasa unapokohoa au kupiga chafya.
👉🏿Usingizi usioeleweka.
👉🏿Kuwa na wasiwasi au hofu.
👉🏿Msongo Wa mawazo.
👉🏿Kukosa hamu au hisia na tendo la ndoa.
👉🏿Mzunguko Wa damu yaan hedhi kuchukua muda mfupi au mrefu.
👉🏿Kutokwa na damu kipindi cha mzunguko.
👉🏿Mifupa kupungua au kukosa nguvu.
👉🏿Nywele kuwa dhaifu na kupotea.
👉🏿Kuota nywele sehemu mbalimbali za mwili kama usoni,shingoni,kifuani,na mgongo Wa juu.
👉🏿Kuuma,kuvimba na kutokwa na maziwa kwenye chuchu.
TIBA YAKE
Hakuna matibabu kamili ya hili tatizo lililoripotiwa ingawa kuna baadhi ya Dawa unaweza kutumia zikasaidia kupunguza baadhi ya dalili na hupatikana hospital au baadhi ya maduka ya Dawa au kwa wataalamu.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.