MICHEZO
Related Content
Related Content
Mlinzi wa Klabu ya ASEC Mimosas, Anthony Tra Bi Tra anatajwa huko Msimbazi kwenda kuziba pengo la Henock Inonga ambaye Taarifa zinaeleza kuwa mwishoni mwa msimu anaelekea AS FAR Rabat ya Morocco.
Nyota huyo raia wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 25 ameiongoza ASEC kutinga hatua ya robo Fainali ya CAF Champions League msimu huu akicheza michezo yote 12 ya ambayo ASEC Mimosas wamecheza kwenye michuano hiyo.
Inaelezwa kuwa Anthony Tra Bi anataka kuondoka ndani ya ASEC mwishoni mwa msimu huu na anataka kwenda kutafuta changamoto baada ya kuitumikia timu hiyo toka mwaka 2021.
