YUSUF MANJI AFUNGUKA DILI LA KUTAKA KURUDI YOUNG AFRICANS

0:00

NYOTA WETU

Mwenyekiti na Mfadhili wa zamani wa Young Africans, Yusuf Manji amesema kwa sasa hafikirii kurejea ndani ya klabu hiyo ingawa anafurahia kuona imekuwa na umoja na mshikamano wa hali ya juu.

Manji amesema kwa sasa umri wake unambana kujiweka karibu na timu hiyo na soka kwa ujumla, hivyo anaendelea kujishughulisha na mambo mengine.



“Kwa sasa siwezi, kwanza umri umeenda siwezi zile pilikapilika za kusimamia timu,” amesema Manji aliyeiongoza Young Africans kwa miaka minne.

“Unajua hata kama utakuwa ofisini, tabia yangu ni kwamba napenda kufanya kazi zote nikiwa karibu. Naweza kuwa na viongozi wengine lakini nitalazimika kusafiri na wachezaji, nahakikisha kila kitu chao kinaenda vizuri, ukweli kwa kipindi hiki sitakuwa na uwezo tena wa kufanya hivyo wanatakiwa kufanya vijana.”



Manji amesema kuwa pamoja na hilo, anafurahia kuona klabu hiyo ina umoja wa hali ya juu kwa sasa jambo ambalo lilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu.



“Moja ya jambo ambalo nakumbuka nililifanya na kuisaidia Young Africans hii kufika hapa ni kuweka umoja, wakati naingia nilikuta migogoro mingi kulikuwa na makundi matatu, nakumbuka moja liliitwa Yanga Asili, lingine Kampuni moja liliitwa Yanga Akademia.

“Nilitumia ushawishi na wangu wote na kuhakikisha haya makundi yanaisha na Young Africans ikasimama, nafikiri imewasaidia hadi leo ndiyo maana kuna umoja,” amesema Manji.

Katika hatua nyingine Yusuf Manji amefunguka sakata la mashabiki kuingia uwanjani bure

“Nilianzisha mfumo wakati mwingine wa kununua tiketi zinaenda kugawiwa kwenye matawi ya Young Africans kwa kuwa nilitaka kurudisha kwa jamii. Kama unakumbuka mchezo wa Young Africans na TP Mazembe mashabiki waliingia bure.”

See also  Mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania mwenye umri wa miaka 20, aliyekuwa akikipiga kwenye klabu ya KRC Genk, Kelvin John amejiunga na klabu ya AaB Fodbold inayoshiriki ligi daraja la kwanza maarufu kama NordicBet Liga ya huko nchini Denmark.

“Pale haikuwa bure kama ambavyo inafanyika sasa, bali nilinunua tiketi zote zikagawiwa kwa mashabiki wa Young Africans kupitia kwa viongozi wa matawi yao. Nia ilikuwa ni kuhakikisha mchezo huu unarudi kwa jamii yetu,” amesema Manji mmoja wa wafadhili wa klabu walioweka rekodi ya kuwa kipenzi cha mashabiki nchini.”

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Leclerc fined for swearing, stewards say Verstappen...
SAO PAULO, - Formula One stewards fined Ferrari's Charles Leclerc...
Read more
Klabu ambazo Ziko Mbioni Kununua Mkataba wa...
Story zinazotrend Nchini ni : ◉ Aziz Ki kuhusu mkataba mpya...
Read more
HOW TO SUCK A DICK
❤ Start by being super hot 🔥🤌Don't suck dìck because...
Read more
Mmiliki tajiri wa vyombo vya habari duniani,...
Murdoch mwenye umri wa miaka 93 amefunga ndoa hiyo jana...
Read more
Liverpool forward Darwin Nunez has been banned...
Nunez, 25, was seen physically confronting Colombia fans in the...
Read more

Leave a Reply