MTAZAMO WA BABA ASKOFU BAGOZA KUHUSU KUKATWA KWA MALISA GJ NA BONIFACE JACOB

0:00

NYOTA WETU

Baba Askofu Benson Bagonza ameandika yafuatayo:”

NCHI HII KUBWA: Bora Taharuki kuliko Mauaji.

Sifa moja muhimu ya kiongozi ni kufanya maamuzi yenye maslahi mapana kwa jamii.

Nyumba inapoungua moto, ni bora kuokoa hata godoro moja kuliko kuua panya wanaokimbia moto unaounguza nyumba.

Mitandao ya kijamii usiku wa leo (25/4/2024) imejaa habari za Mwanaharakati wa haki za kijamii Malisa GJ na Mwanasiasa/Mwanaharakati Jacob Boniface kukamatwa na polisi kwa KUSABABISHA TAHARUKI wakati wanaripoti “mauaji” ya mtu mmoja aitwaye Robert Mushi.

Kama ningelikuwa jeshi la polisi ningetafakari haya kabla ya kufanya maamuzi:

  1. Nchi hii ni kubwa sana. Jeshi la polisi ni dogo kuliko uhalifu. Wanaojitolea kutoa taarifa za uhalifu ningewafanya marafiki kuliko maadui.
  2. Ni kweli Robert Mushi amekufa. Ningeshughulika na wauaji kuliko kushughulika na waliosababisha taharuki.
  3. Ningejiuliza; taharuki imesababishwa na ripoti ya kifo au kifo chenyewe? Kifo kisicholeta taharuki si kifo kamili.
  4. Malisa GJ ameisharipoti matukio mengi ya kihalifu ambayo jeshi la polisi ama halikujua au lingepata taabu sana kujua. Kwa hili la kifo cha Robert Mushi, Jeshi la polisi lingemzawadia nishani ya utumishi wa kujipendekeza kwa polisi kuliko kumkamata na kumpekua.
  5. Badala ya kumpekua Malisa GJ na Boniface Jacob, ningewatumia na mitandao yao kutafuta na kujua gari linalodaiwa kumgonga marehemu Moshi.
  6. Kwa kuwa nchi ni kubwa sana; ningetumia muda kuchunguza ndani na nje ya jeshi la polisi kuhusu uwezekano wa polisi vishoka wanaodaiwa kumkamata marehemu Robert Mushi kabla ya kifo chake!
  7. Ningeazimia kuwalinda wanaojitolea kutoa taarifa za uhalifu kuliko wanaodaiwa kukosea katika kutoa taarifa za uhalifu ili kwa njia hiyo niongeze wigo wa watoa taarifa za uhalifu.
See also  PALESTINA SASA RASMI AMETAMBULIKA KAMA NCHI HURU

Lakini kwa kuwa mimi si Jeshi la polisi bali ni mtu ninayejifanya Askofu wakati hata uaskofu umenishinda, nabakia kutamani kuwa polisi huku nikijua kuna polisi wanatamani kuwa Askofu.

Natamani Jeshi la polisi liwaachie huru Malisa GJ na Boniface Jacob ili linufaike na harakati zao katika kukomesha uhalifu wa kidola na kiraia”.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

NYOTA WA MIELEKA VIRGIL JONES AFARIKI DUNIA
NYOTA WETU Nyota wa Mieleka wa Marekani Michael Jones (61)...
Read more
Christ Embassy church in Lagos erupted by...
On Sunday morning, a fire erupted at the Christ Embassy...
Read more
RISK OF HAVING SEX EVERYDAY
LOVE TIPS ❤ 1. PAIN IN THE PENISyou can develop...
Read more
Porto's Gonzales hands MVP award to ball...
Porto midfielder Nico Gonzalez, who assisted in the winning goal...
Read more
STRATEGIC DOCUMENTS A BUSINESS SHOULD HAVE
BUSINESS 12 STRATEGIC DOCUMENTS A BUSINESS SHOULD HAVE 1. Business...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply