MICHEZO
Klabu ya Young Africans ipo kwenye mpango wa kumuongezea mkataba mpya wa mwaka mmoja kiungo wao Jonas Mkude mwenye umri wa miaka 31, ambaye anamalizia mkataba wake mwishoni mwa msimu huu.
Mkude alisajiliwa na Young Africans kama mchezaji huru mwanzoni mwa msimu huu baada ya mkongwe huyo kutemwa na Simba SC aliyokuwa ameitumikia kwa takribani miaka 13.
Young Africans walimpa Mkude mkataba wa mwaka mmoja kwa kuwa hawakuwa na uhakika kama angeweza kuwa na kiwango bora hasa ikikumbukwa kuwa hakuwa akipata nafasi ndani ya Simba SC kwa muda mrefu katika kipindi cha mwaka wake wa mwisho ndani ya timu hiyo.
Mkude ameonesha uwezo mkubwa katika mechi za hivi karibuni hasa zile za Kimataifa (Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika) dhidi ya Mamelodi Sundowns ya nchni Afrika Kusini, jambo lililowafanya viongozi wa Young Africans wafikirie kumuongezea kandarasi nyingine.
Related Posts 📫
Post does not have featured image