RAIS SAMIA ATANGAZA NEEMA KWA WABUNIFU NCHINI

0:00

SIASA

Wizara ya Nishati imetakiwa kuwatafuta Watanzania Wabunifu wa teknolojia, ili waweze kufanikisha mpango wa matumizi ya gesi ya kupikia kwa kulipia kadri unavyotumia.

Wito huo umetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akiuzindua Mkakati wa Taifa wa nishati safi ya kupikia wa mwaka 2024 Jijini Dar es salaam.

Amesema, “watuletee pia teknolojia rahisi itakayowezesha Wananchi kupata nishati safi kadri ya uwezo wao kwa mfano kulipia kadri anavyotumia kama inavyofanyika kwa umeme na maji, zile pre paid meters.”

Aidha, Rais Samia ameongeza kuwa, “tunalo jukumu la kuongeza uelewa kwa Wananchi kuhusu nishati safi ya kupikia na kutunga sera nzuri na wezeshi, ili kufikia malengo ya mkakati huu, katika hili wenzetu wa Wizara ya Nishati watatuongoza kuhakikisha nishati safi ya kupikia inapatikana kwa uhakika na kwa bei inayohimilika kwa Wananchi.”

Hata hivyo ameongeza kuwa moja kati ya maonesho ya mazingira aliyowahi kutembelea aliwahi kuikuta teknolojia hiyo ambapo Watanzania walitengeneza mitungi ambayo unatumia gesi jinsi unavyolipa.

“Unachukua mtungi mzima kama umelipa elfu 10 utatumia gesi yako ya elfu 10 ikimalizika mtungi unakata hata kama gesi ipo mpaka uwasiliane nao tena ulipe tena wakufungulie utumie tena naomba sana watafute au kama wapo wajitokeze tufanye nao kazi,” alisisitiza Rais.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Chory double leads Czechs to 2-0 Nations...
PRAGUE, - Tomas Chory scored in each half to lead...
Read more
CLEMENT MZIZE NA PRINCE DUBE WAZIKUTANISHA KATI...
MICHEZO Wakati tetesi zikieleza kuwa Uongozi wa Azam FC umewasilisha...
Read more
AINA ZA UTE UKENI NA MAANA YAKE
Ute ukeni hutofautiana kwa rangi, muonekano, na harufu kulingana na...
Read more
WATANZANIA VINARA WA AKILI AFRIKA
MAKALA
See also  FREEMAN MBOWE MWANASIASA,MFANYABIASHARA NA MKULIMA ASIYE OGOPA HASARA
Ripoti ya nne ya 'Global Mind Project' kuhusu 'Hali...
Read more
Tragedy has struck the world of football...
Reports indicate that Obi was positioned at the front of...
Read more

Leave a Reply