HABARI KUU
Kwa mujibu wa matokeo ya awali ya Tume ya Uchaguzi, Rais wa mpito wa Chad, Mahamat Idriss Déby Itno, ameshinda uchaguzi wa Urais wa Mei 6 kwa asilimia 61.03 ya kura, mbele ya mpinzani wake mkuu, Waziri Mkuu Succès Masra, aliyepata kura 18.53%.
Hata hivyo Bw.Masra amedai kushinda uchaguzi huo katika raundi ya kwanza.
Waziri Mkuu wa zamani Albert Pahimi Padacé amekamata nafasi ya tatu akipata kura 16.91% kiwango cha walioshiriki uchaguzi ikiwa ni 75.89%, kulingana na tume ya uchaguzi.
Matokeo ya muda ya uchaguzi wa urais wa Jumatatu nchini Chad yalitangazwa na Kiongozi wa Tume ya Uchaguzi Alhamisi jioni, Mei 9, siku 12 kabla ya tarehe iliyopangwa ambapo matokeo hayo yanatarajia kuthibitishwa na Baraza la Katiba nchini humo kama matokeo rasmi.