Burundi yaishutumu Rwanda kuhusika na shambulio la Bujumbura

0:00

HABARI KUU

Burundi imeishutumu Rwanda kuhusika katika shambulio la guruneti ambalo liliwajeruhi watu 38 karibu na Soko Kuu la zamani mjini Bujumbura.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama Pierre Nkurikiye amefahamisha kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakipata mafunzo nchini Rwanda kupitia kundi la waasi la Red Tabara ambalo limekuwa liishambulia Burundi.

Amesema kuwa watu sita wamekamatwa Kwa shutuma za kuhusika na shambulio hilo,uchunguzi ukiwa unaendelea kufanyika ili kuwabaini watu wengine.

Hilo linakuwa shambulio la pili baada ya lililotokea maeneo ya Kamenge wiki moja iliyopita na kujeruhi watu sita, mmoja akipoteza maisha baada ya kufikishwa hospitalini.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

TOOLS, SKILLS AND DOCUMENTS EVERY MARKETER SHOULD...
Marketing Strategy: This document should outline the overall marketing goals and...
Read more
MBINU 10 ZA KUONGEZA WINGI WA MBEGU...
Mwanaume mwenye uwezo wa kuzalisha anahitaji kuwa na mbegu zisizopungua...
Read more
SABABU MARIOO KUFUNGULIWA KESI
NYOTA WETU Msanii Toto Bad maarufu kama @marioo_tz amefunguliwa kesi...
Read more
TWIGA STARS YAFUZU KUCHEZA WAFCON 2024 ...
MICHEZO Timu ya soka ya wanawake ya Twiga Stars imefuzu...
Read more
KURASA ZA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 23,2023...
Magazeti https://www.kotobee.com?aff=ac74a Karibu Mtanzania kwenye magazeti ya leo kwa njia ya...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Kuna Ukweli Gani Kuhusu Afya ya Joe Biden?

Leave a Reply