MANCHESTER CITY SASA NI RASMI KUBEBA UBINGWA

0:00

MICHEZO

Ushindi wa mabao 2-0 walioupata Manchester City dhidi ya Tottenham Hotspur katika uwanja wa ugenini umewafanya wajiweke katika mazingira mazuri zaidi ya kulitwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza (English Premier League).

Mabao ya Manchester City katika pambano hilo gumu la yamefungwa na mshambuliaji wake kinara wa ufungaji mabao Erling Haaland katika kipindi cha pili cha mchezo huo.

Ushindi huo umevunja matumaini ya Arsenal kukitwaa kikombe hicho ambacho mara ya mwisho walikitwaa Mwaka 2004.

Ushindi huo wa Manchester City umewafanya wafikishe pointi 86 na kushika usukani wa ligi hiyo na kuwaacha Arsenal wakiwa nafasi ya pili na pointi zao 86, huku timu hizo zikiwa na michezo 37 kila mmoja.

Michezo ya mwisho ya timu hizo ndiyo itakayoamua bingwa atakuwa nani. Arsenal watakuwa nyumbani kwao Emirates Stadium kucheza dhidi ya Everton, huku City nao watakuwa nyumbani kwao Etihad Stadium kucheza dhidi ya West Ham.

Kama City watafanikiwa kushinda kikombe hicho watakuwa wameshinda mara nne mfululizo wakiwa chini ya kocha wao Pep Guardiola.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MOHAMED SALAH AWAGOMBANISHA LIVERPOOL NA EFA ...
MICHEZO Suala la afya ya Mohamed Salah limeibua mvutano kati...
Read more
Kenyan Environment CS Nominee Aden Duale Discloses...
Aden Duale, the nominated Environment, Climate Change and Forestry Cabinet...
Read more
RAIS WA HUNGARY AJIUZULU WADHIFA WAKE
HABARI KUU Rais wa Hungary amejiuzulu kutokana na ghadhabu ya...
Read more
Ufahamu Mkoa Wa Singida Nchini Tanzania
Mkoa wa Singida ulianzishwa rasmi Oktoba 15, 1963 ambapo kabla...
Read more
YOUNG AFRICANS YATINGA ROBO FAINALI IKIICHAPA DODOMA...
MICHEZO
See also  Mauricio Pochettino hana presha ndani ya Chelsea
Wananchi, Young Africans Sc wametinga hatua ya robo fainali...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply