JKT IPO MBIONI KUACHANA NA MATUMIZI YA KUNI HUKU SABABU IKITAJWA

0:00

HABARI KUU

“JKT TUKO TAYARI KUTEKELEZA, MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA”

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema kuwa wapo asilimia 98 ya kuhakikisha kwamba matumizi ya Nishati ya Kuni na Mkaa yanapotea ndani ya Jeshi lao la JKT

Meja Jenerali Mabele ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika kikosi Cha Jeshi 822 Rwamkoma JKT Kilichopo Wilayani Butiama Mkoani Mara

Meja Jenerali Mabele amesema kuwa Serikali inapotoa maelekezo wao kama Jeshi wanakuwa watu wa kwanza kuyatekeleza maagizo hayo na wapo tayari wakati wote Kwa ajili ya maelekezo

Meja Jenerali Mabeyo ameongeza Kwa kusema kuwa tangu Serikali walipoanza kuzungumza kuhusu matumizi ya Nishati safi ya Kupikia wao waliona ni maagizo na hata kabla ya maelekezo hayajatolewa wao walishaanza kuyafanyia kazi kutokana huo ndio utaratibu wao wa maisha

Kwa upande wake Kamanda Kikosi Cha Rwamkoma JKT Luteni Kanali Gaudencia Mapunda amesema kuwa manufaa wanayoyapata katika matumizi ya Nishati safi ya Kupikia ni utunzaji wa Muda na hata vijana wanaopika katika majiko hayo hawaathiriki na Moshi tofauti na kipindi Cha nyuma wakati walipokuwa wakitumia Nishati chafu ya Kupikia.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MICHAEL OLISE KWENYE RADA ZA MANCHESTER UNITED
MICHEZO Klabu ya Manchester United imewekeza nguvu kubwa zaidi kwenye...
Read more
FREEMAN MBOWE MWANASIASA,MFANYABIASHARA NA MKULIMA ASIYE OGOPA...
Miaka 64 iliyopita familia moja ya kitajiri mkoani Kilimanjaro ilipata...
Read more
MFAHAMU MSANII AYRA STARR WA NIGERIA
MICHEZO/BURUDANI Staa mwimbaji wa muziki wa Afrobeat kutoka Nigeria Ayra Starr...
Read more
𝘽𝙪𝙨𝙞𝙣𝙚𝙨𝙨 𝙋𝙖𝙧𝙩𝙣𝙚𝙧𝙨𝙝𝙞𝙥𝙨; 𝙩𝙝𝙞𝙣𝙜𝙨 𝙮𝙤𝙪 𝙣𝙚𝙚𝙙 𝙩𝙤 𝙠𝙣𝙤𝙬...
For us to properly discuss partnerships, we must first define...
Read more
KENYA KUTOA VISA YA DUNIA ...
HABARI KUU.
See also  Nikki Haley kumpigia Donald Trump kura
Rais wa Kenya, Dkt. William Ruto amesema kuanzia...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply