MAKALA
–
Kwa miaka mingi sana tumekuwa tukimtazama Sana diamond platnumz kuwa ndio msanii pekee mwenye mabavu ya kuufanya mziki wetu kufika kimataifa imekuwa tofauti na mtazamo yetu.
Siku hizi diamond platnumz amekuwa msanii wa kisujudia radha ya mziki wa Amapiano na kuitupa mbali Bongo Fleva, Kwa muktadha huo inamaanisha diamond platnumz ameamua kutusaliti sisi watanzania na kupromote mziki wa Madiba “Amapiano”.
Ukiangalia mtu kama Asake hakutaka kabisa kupoteza Identity ya Afrobeat aliamua kuchanganya Amapiano na Afrobeat “Afropiano” bila kiathiri vionjo ya mziki wa nchini mwao, Ila tumaini letu amekuwa mstari wa mbele kabisa kuua mziki wetu.
Kwasasa diamond platnumz ameanza kupoteza mvuto kabisa kwenye tasni hii ya Bongo Fleva ndio maana ameanza kijiwekeza kwenye vitimbwi vya Nje ya mziki. Kwa Upande wangu Kwa Sasa Nedy Music ni msanii mkali Kuliko diamond platnumz.