Kitisho cha Ziwa VICTORIA kuumeza Mkoa Kagera

0:00

HABARI KUU

Mkazi wa Manispaa ya Bukoba Mzee Pius Ngeze (70), amesema anahofia balaa kubwa kutokea katika Mkoa huo kumezwa na ziwa Victoria, kutokana na kukosekana kwa mikakati mahsusi wala uchunguzi, ili kubaini kwanini Tetemeko, Mafuriko na majanga mengine yanatokea mara kwa mara na kusababisha athari kwenye jamii.

Ngeze ambaye pia ni mmoja wa Wazee washauri wa Mkoa huo, amesema hata mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia Ijumaa ya Mei 10, 2024 ilisababisha Mafuriko katika maeneo mbalimbali, lakini hakuna tamko la watafiti la kuipanga jamii katika makazi rasmi, ili kukwepa maafa zaidi ya kupewa tahadhari pekee.

Amesema, “ndani ya Mkoa Kagera Manispaa ya Bukoba mafuriko yamesababisha adha kwa wakazi nikiwemo mimi kwani vitabu ninavyozalisha na mali zilizokuwa ndani ya nyumba zenye thamani ya milioni 100, zimeharibika na kukosa sifa zikiwemo nyaraka na vitabu. Nani atatuambia kuhusu hili mana hali imezidi kuwa mbaya Kagera kila siku matukio.”

Mzee Ngeze ameongeza kuwa, Serikali inatakiwa kutoka na sera, ili kuwashirikisha Wananchi katika ujenzi wa makazi yatakayostahimili matetemeko na kukwepa mabonde kuepuka maafa, kwani Bukoba kila mwaka hupita matetemeko madogo madogo yasiyopungua 20, vimbunga vya majini hadi nchi kavu hali ambayo haijawahi kutokea.

“Ninahoji kama mwananchi wa kawaida, hii hali ya Ziwa kujaa kiangazi na matetemeko kuja kila baada ya miezi miwili vina uhusiano gani? sikupata jibu la kuridhisha lakini niliwahi kumuambia Mkuu wa Mkoa na RAS wakahi huo jambo hili lakini kama hawatafanyia kazi hili hali inazidi kutisha.

Dhoruba wakati wa msimu wa mvua si jambo geni lakini kwa mwaka huu, mvua kubwa zimeshuhudiwa kutokana na mfumo wa hali ya hewa wa El-nino, huku Wataalamu wakisema mabadiliko ya tabianchi pia yamechochea hali hiyo ambayo imeleta madhara maeneo mengi.

See also  Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa ana uhakika wa ushindi katika Mdahalo wake utakaofanyika Juni 27 dhidi ya Rais wa sasa wa taifa hilo Joe Biden.
Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Clatous Chama aipa "Thank you "Simba kikubwa
Ni takribani kilomita 0.6 ametumia Clatous Chama kutoka Makao...
Read more
CBN raises interest rate to 26.75%
The Central Bank of Nigeria, CBN, Monetary Policy Committee, MPC,...
Read more
YUSUF MANJI AFUNGUKA DILI LA KUTAKA KURUDI...
NYOTA WETU Mwenyekiti na Mfadhili wa zamani wa Young Africans,...
Read more
POLISI AKODI MAJAMBAZI
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
CHIELLINI AMESTAAFU KUCHEZA MPIRA
NYOTA WETU. Beki wa zamani wa Juventus na Timu ya...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply