Rodrigo afichua siri ya Arsenal kukosa Ubingwa wa EPL

0:00

MICHEZO

Kiungo kutoka nchini Hispania Rodrigo Hernández Cascante ‘Rodri’ amefichua wapi Arsenal walipokosea katika mbio za kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu wa 2023/24.

“Mojawapo ya mechi hizo ni ile ya sare tasa katika uwanja wa Etihad mwishoni mwa mwezi Machi ambayo ilishuhudiwa Arsenal wakiwa na asilimia 27 pekee ya kumiliki mpira huku wakitunyima ushindi.

“Kwa hakika Arsenal walistahili kutwaa Ubingwa kwa sababu walikuwa na kikosi imara, ila tukubali walianza kukosea kwenye mchezo waliocheza hapa dhidi yetu.

“Walipofika hapa walitukabili vilivyo, lakini niliona dhumuni lao lilikuwa ni kutafuta sare badala ya kushinda, nilipoona hilo nilibaini hawa hawataweza kufikia lengo la kuwa mabingwa msimu huu.” amesema Rodri

Arsenal iliyokuwa na Kikosi Bora msimu wa 2023/24 ilionesha kupambana katika mbio za ubingwa hadi kwenye michezo ya mwisho iliyopigwa jana Jumapili (Mei 19), huku ikishinda 2-1 dhidi ya Everton na Man City ikiifunga West Hama United 3-1.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Klabu ya Singida Black Stars (zamani Ihefu Fc) imethibitisha kuingia makubaliano na aliyekuwa kocha wa Simba Sc, kocha Kocha Patrick Aussems raia wa Ubeligiji kuwa Kocha Mkuu klabuni hapo kuanzia msimu mpya wa 2024/25 kwa kandarasi ya awali ya msimu mmoja mpaka tarehe 30 Juni 2025.
Don't miss out!
Invalid email address

By Mujuni Henry

JUNIITV

Please disable your adblocker or whitelist this site!

         banner                            

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading