Newcastle United kumsajili Giorgi Mamadashvili

0

0:00

MICHEZO

Klabu ya Newcastle United inaandaa ofa ya kumsajili Mlinda Lango wa Valencia, Giorgi Mamadashvili.

Kipa huyo kutoka nchini Georgia anatarajiwa kuuzwa na Los Che msimu huu wa majira ya joto.

Gazeti la The Times limeripoti kuwa, Newcastle wana nia ya kumpeleka Mamadashvili nchini England, ili kumpa changamoto Mlinda Lango wao wa sasa Nick Pope.

Mamadashvili kwa sasa anatazamwa kuwa miongoni mwa Walinda Lango bora kwenye Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’.

Valencia inahitaji Pauni Milioni 35, ili kuafiki dili la kumuuza Mlinda Lango huyo mwenye umri wa miaka 23.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Onyeka Onwenu: Family hails Peter Obi for staying with music icon till her last moments
Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading