HABARI KUU
Nchini Afrika Kusini, chama cha umkhonto wesizwe sasa kinasema kuwa kiongozi wake rais wa zamani, Jacob Zuma , atatumia mbinu zote zilizopo ikiwemo kwenda katika kamati ya haki za binadamu ya umoja wa mataifa, kuhakikisha uamuzi wa hapo jana wa mahakama ya kikatiba unabatilishwa.Mahakama ya Katiba nchini Afrika Kusini katika uamuzi wake imesema kuwa Jacob Zuma haruhusiwi kugombea katika Uchaguzi mwishoni mwa mwezi huu.
Mahakama imeeleza kuwa Katiba inamzuia raia yeyote aliyehukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi 12 jela kuwania nafasi katika uchaguzi.
Zuma, ambaye aliondoka madarakani mwaka 2018 akiwa anakabiliwa na tuhuma za rushwa, alipatikana na hatia ya kudharau maagizo ya Mahakama mwaka 2021 na kuhukumiwa kifungo cha miezi 15 jela.
Kufuatia uamuzi huo, Tume huru ya uchaguzi imesema kuwa karatasi za kupigia kura sasa hazitachapishwa tena ikiwa imesalia siku tisa kabla ya zoezi la kupiga kura mwezi huu.
Katika uamuzi wake, mahakama hiyo iliamua kuwa Zuma hawezi kuchaguliwa kuingia bungeni, kutokana na kifungo cha miezi 15 jela alichopewa 2021 kwa kukosa kuheshimu mahakama.
Tume ya uchaguzi ilikuwa imeeleka kwenye mahakama hiyo kutafuta ufafanuzi kuhusu kipengee cha katiba kinachomzuia mtu kuwania wadhifa wowote ikiwa amewahi kuhukumiwa kifungo jela.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.