HABARI KUU
Maelfu ya watu wamekusanyika katikati mwa mji mkuu wa jimbo la Azerbaijan Mashariki, wakiomboleza huku wakiwa wamebeba picha za aliyekuwa rais wa Iran, Ebrahim Raisi aliyefariki katika ajali ajali ya Helikopta.
Katika ajali hiyo, Ebrahim Raisi (63), aliaga dunia sambamba na Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi hiyo, Amir Abdollahian na Maafisa wengine saba wa Serikali.
Mwili wa Raisi, Waziri wake wa Mambo ya Nje na watu wengine waliokuwemo kwenye helikopta hiyo yatapelekwa Qom kisha jijini Tehran ambapo kutakuwa na utoaji wa heshima za mwisho.
Kiongozi Mkuu wa Taifa hilo, Ayatollah Ali Khamenei atatangaza sala ya mazishi ambapo waumini wataungana na Viongozi wa kigeni ili kushiriki zoezi hilo muhimu.
Taarifa za Waislamu wengi wa Kishia nchini Iran, wanasema mwili wa Rais utapelekwa Mashhaa, eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo kwa ajili ya mazishi, kwenye kaburi la Imam Reza, mrithi wa nane wa Mtume Muhammad.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.